Hali katika uwanja wa Majimaji, maarufu kama wanalizombe
ulianza kufurika majira ya saa nne asubuhi, baada ya wananchi hao wengi wakiwa
vijana kumaliza shughuli za ibada kutoka makanisani.
Mratibu wa tamasha hilo kwa niaba ya Kilimanjaro Premium
Lager, Amedeo Thadeo, alisema kwamba wameamua kufanya bonanza hilo katika mji
wa Songea baada ya kubaini kuwa mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa yenye mashabiki
wengi wa vilabu vya Simba na Yanga.
Hata hivyo, michezo kadhaa iliyoanza kufurahisha wananchi
waliofurika katika uwanja huo ulikuwa wa kufukuza kuku tena Jogoo, ambapo
washiriki wawili wapenzi wa klabu za Simba na Yanga walishirikishwa baada ya
kuvalishwa jezi za vilabu hivyo.
Lakini kwa bahati mbaya, wapenzi wa Simba, walishindwa
kuongeza furaha yao katika uwanja huo, baada ya mshiriki wao kushindwa kumaliza
mbio hizo kwa mafanikio, huku yule wa Yanga Deogras Mwanji, akiibuka kidedea
baada ya kufanikiwa kumkamata jogoo huyo baada ya dakika mbili na sekunde 25.
Hata hivyo, Mwakilishi wa Mauzo TBL mkoani Ruvuma Masoud
Mrisho, aliliambia gazeti hili kwamba mwamko ulikuwa mkubwa uwanjani hapo,
baada ya vijana walikuja kutoka Dar es Salaam kufanya maonyesho ya promosheni
kadhaa kwenye baa kadhaa mjini Songea.
“Walipokuja hapa Songea wasanii waliosimamia bonanza hili
walianza na kuendesha promosheni katika baa ya Serengeti, Yapenda Mtini, Delux
II, Mamboleo na kumalizia katika baa ya VALONGO VANGU, mjini Songea na kupata
uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa jamii,” alisema Masoud.
Masoud alisema wananchi wengi walikuwa na shauku kubwa la
bonanza, hivyo kila kona alikopita yeye na wenzake, walitakiwa kuwahakikishia
kwamba bonanza hilo litafanyika bila kukosa, huku wanenguaji kutoka Bendi za
Akudo Impact Chicharito, na Afande aka Mjeda na Queen Lucy aka Mama Mdogo
wakilipamba jukwaa na kuwaburudisha ipasavyo wananchi waliofurika uwanjani
hapo.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kwamba
shughuliza kijamii katika mji wa songea zilisimama kwa muda kutokana na bonanza
hilo, hali ambayo ilionyesha kuwa wananchi wengi walikuwa na shauku kubwa na
bonanza hilo, japo kuwa wasanii wenyeji wa mji wa Songea walishindwa kuonyesha
umakini wao baada ya kupatiwa nafasi ya kusherehesha jukwaa.
Waliozungumza na gazeti hili waliipongeza Kilimanjaro
Premium Lager kwa bonanza hilo na kusema limeamsha hamasa ya kimichezo mkoani
humo, ambayo imepotea baada ya timu ya Maji Maji iliyokuwa ikishiriki Ligi Kuu
ya Tanzania kwa miaka kadhaa, lakini ikajikuta ikishushwa daraja baada ya kushindwa
kufanya vizuri.
Bonanza hilo lililoshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea,
Joseph Mkirikiti, alionyesha dhahiri ni mshabiki wa Yanga, alipoingia uwanjani
alikabidhiwa jezi ya klabu ya Yanga, na aliamua kusalimia wananchi wote kwa
kluzunguka na kupunga mikono na kuamua
kwenda moja kwa moja kukaa katika jukwaa kuu la uwanja huo, na kuwapongeza
wananchi waliojitokeza katika bonanza hilo akisema amefurahishwa na uratibu wa
bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa shughuli hiyo.
Kikosi cha timu ya yanga
Umati wa watu wakiangalia michezo iliyo kuwa ikiendelea katika uwanja wa majmaji kushuhudia bonanz kupitia kampeni ya nini mtani jembe.
Mashabiki wa yanga na simba wanawake wakishindana mchezo wa kuvuta kamba katika bonanza la nani Mtani jembe lililo fanyika katika uwanja wa majimaji.
Mashabiki wa simba wakishangilia baada ya kuwashinda yanga mchezo wa kuvuta kamba kupitia bonanza la nani mtani jembe
No comments:
Post a Comment