Mbio maalum za mwenge wa uhuru Wilaya ya Magu zilizofanyika 03.07.2021 na kuifikia miradi kumi na moja, miradi sita ilikusudiwa kuzinduliwa, mitatu imekaguliwa na miwili iliwekewa mawe ya msingi.
Mapema jana Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kalli alipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bi.Senyi Ngaga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema aliye mwakilisha Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa mkoa wa Mwanza ambaye yuko safari kikazi nje ya mkoa.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Wilaya DC Kalli wakati akimkaribisha kiongozi wa mbio maalum za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2021 Luteni Josephina Paul Mwambashi alisema kuwa miradi yote itakayopitiwa na mwenye wa uhuru ina jumla ya Tsh.5,210,528,538.00.
MIRADI.
Mradi wa kwanza ni Ujenzi wa Shule ya Sekondari Bugatu uliofadhiliwa na kampuni ya Alliance Ginneries Ltd kwa Tsh.166,145,500.00 ‘ Ujenzi wa shule hiyo umewapunguzia umbali mrefu wa kilomita 16 waliokuwa wakisafiri wanafunzi kutoka vijiji vya Salama, Bugatu na Chandulu. Katika mradi huu Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa aliipongeza sana Kampuni ya Alliance kwa mchango wake katika maendeleo ya Elimu na kuitunuku Hati ya Pongezi iliyopokelewa Meneja wa kampuni hiyo ya kuchambua pamba.
Mradi wa pili ni Lishe –Bugatu ambapo kiongozi wa mbio za Mwenge baada ya kupokea taarifa ya hali ya lishe na udumavu wa watoto alizundua mrdai huo na kusisitiza elimu iendelee kutolewa kwa jamii.
Mradi wa Tatu uliozinduliwa ni Klabu ya kupambana na kuzuia rushwa –Bugatu, uzinduzi ulifanyika sambamba na hati ya utambuzi wa kilabu ilitolewa.
Mradi wa nne ni uzinduzi wa Mradi wa Maji bomba Kijiji cha Ng’haya wenye thamani Tsh.309,439,538.00, mradi umekamilika na maji wananchi wanapata na umeweza kutoa huduma kwa wanatumiaji maji 840. Iligizwa kuwa nyaraka husika za mradi kuhakikisha zinakalimilika mara moja.
Mradi wa tano ni Mradi wa Tehama wa shule ya Sekondari Magu wenye thamani ya Tsh.23,950,000.00, Mradi unashirikisha shule za Lugeye na Magu ambapo wameanzisha Maktaba ya kidigital ambayo imehifadhi nakala tete za Notes, vitabu,mitihani iliyopita pia mfumo wa masomo kwa njia ya masafa Mwalimu wa Lugeye SS anaweza kufundisha wanafunzi walioko Magu SS kwa njia ya video, pia mradi huo unaweza kusaidia kuendesha mikutano kwa njia ya mtandao hasa kipindi hiki cha UVIKO 19.
‘Kiongozi wa mbio maalum za mwenge amepongeza mradi huu na kusema kuwa unaweza pia kusaidia kukabiliana na upungufu wa walimu hasa wa masomo ya sayansi lakini mradi ulipongezwa kwa vile unaendana kabisa na kaulimbiu ya mwenge isemayo ‘TEHAMA NI MSINGI WA TAIFA ENDELEVU ITUMIE KWA USAHIHI NA UWAJIBIKA’.
Miradi mingine ni Uzunduzi wa barabara Karume –Ilungu wa Tsh.15,459,000.00 na uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa jengo la zahanati Ilungu, Mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba, Kisima kirefu cha Maji cha Lubangida, Mradi wa watu wenye ulemavu Isangijo na mpango kuthibiti malaria maarufu kama ZIRO MALARIA –uliofanyika zahanati ya Isangijo.
Hatimaye Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kalli amekabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Elias Masala leo 04.07.2021 kwa ajili kuendelea ratiba ya mbio maalum mwenge 2021.
'Kazi iendelee'
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Magu
Habari, mawasiliano na itifaki.
+255 716 094 601
No comments:
Post a Comment