Saturday, May 11, 2013
FUMANIZI LA PADRI
LILE saga la madai ya fumanizi la Padri Urbanus Ngowi aliyekuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishiwa Makomu, Marangu limeibua mtikisiko mkubwa kwa Kanisa Katoliki nchini, Risasi Jumamosi lina mapya yaliyoibuka.
KWANI ILIKUWAJE?
Katika habari iliyofichuliwa na gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda, toleo namba 313 la Jumatatu, Aprili 29 hadi Mei 5, mwaka huu, ilidaiwa kuwa Father Ngowi alinaswa chumbani akiwa na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la kijamii la Mama P.
Mara baada ya ‘mzigo’ huo kuingia mitaani nchi nzima, mhariri wa gazeti hilo (jina linahifadhiwa) alianza kupokea simu na ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kutoka kona mbalimbali kwa watu waliojitambulisha kuwa ni waumini wa kanisa hilo wakidai kushtushwa na tukio hilo.
VIKAO VIZITO
Habari za ndani kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi zilieleza kuwa baada ya ishu kuwa ‘hoti’, viongozi wa jimboni hapo, Jumatatu iliyopita walikaa vikao vizito kulijadili suala hilo na kulitolea uamuzi.
Ilidaiwa kuwa uongozi ulikubaliana kumwita mume wa Mama P ambaye wakati tukio hilo likitokea alikuwa jijini Dar es Salaam kwa shughuli zake binafsi.
Ilisemekana kuwa waliwasiliana na mwanaume huyo ambaye alitakiwa kuondoka Dar, Alhamisi iliyopita kwenda Moshi kukutana na viongozi hao kwa lengo la kuweka mambo sawa.
Ilidaiwa kuwa jamaa huyo ambaye amezaa na Mama P watoto wawili, alikubali kukutana na viongozi hao kwa shingo upande huku akitishia kulipeleka suala hilo mbele zaidi kwa kuwa alishalalamika muda mrefu kwamba Father Ngowi ana ukaribu wenye maswali mengi na mkewe.
Risasi Jumamosi lilitonywa kuwa baada ya mwenye mke huyo kulalama sana, Father Ngowi aliitwa na uongozi wa jimbo hilo kisha akaonywa lakini hakuna kilichobadilika.
AHADI NI DENI
Ili kujua uamuzi uliofikiwa ambao Mwakilishi wa Mkuu wa Jimbo la Moshi, Father Paul Uria alimuahidi Mhariri wa Ijumaa Wikienda kuwa Jumatatu iliyopita saa 10:00 angemweleza, alipigiwa simu ambapo mambo yalikuwa hivi:
Mhariri: Pole na majukumu Father Uria.
Father Uria: Nashukuru, nazungumza na nani?
Mhariri: Mimi ni yule mhariri wa magazeti ya Global Publishers (akitajiwa jina) ambaye tulizungumza Ijumaa iliyopita juu ya lile tatizo la Father Ngowi.
Father Uria: Naam, unasemaje?
Mhariri: Uliniahidi nikupigie simu leo muda huu ili uniambie jimbo limefikia uamuzi gani juu ya suala hilo baada ya kukaa kikao.
Father Uria: Nipo njiani naendesha gari (akakata simu).
Saa moja baadaye, Father Uria alipigiwa tena simu lakini iliita bila kupokelewa.
UJUMBE MFUPI
Baadaye alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kupitia simu yake ya kiganjani lakini hakujibu.
Mambo yalipogonga mwamba kwa Father Uria, alipigiwa Father Ngowi ili kujua mustakabali wake juu ya sakata hilo, akawa anakata simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi naye hakujibu.
JUMANNE WIKI HII
Kesho yake (Jumanne iliyopita), Father Uria alipigiwa simu kwa namba tofauti, alipopokea na kusikia utambulisho wa mpigaji kutoka Global Publishers alikata simu na alipopigiwa mara nyingine hakupokea.
Kwa upande wake, Father Ngowi naye alipokea bila kusema chochote, akasikilizia anayepiga na aliposikia utambulisho alikata simu.
MUME WA MAMA P ASAKWA
Risasi Jumamosi huwa halikwepeki, lilimsaka kwa udi na uvumba mume wa Mama P (Mama Peter), Bw. Pasian Mallamsha ambapo Jumatano iliyopita alijaa kwenye kumi na nane na kueleza ya moyoni mwake kuhusu tukio la mkewe na Father Ngowi.
Kwanza mwanaume huyo alikiri kwa njia ya simu kuwa, Mama P ni mkewe na ‘P’ ni herufi ya kwanza ya jina la mmoja wa watoto wao aitwaye Peter.
BOFYA HAPA KUMSIKIA BABA PETER
“Kwanza nashukuru kwa kunipigia. Nimesikia kilichotokea na ni kweli nimeitwa jimboni Moshi kwa hiyo naelekea huko kusikia walichoniitia.
“Kilichotokea kimedhihirisha malalamiko yangu ya muda mrefu juu ya Father Ngowi niliyokuwa nikiyapeleka pale jimboni. Ngoja nikawasikilize lakini lazima kieleweke,” alisema mwanaume huyo.
Risasi Jumamosi lilimuomba Baba Peter kukutana naye uso kwa uso kwa ajili ya mahojiano zaidi lakini ilishindikana kwa kuwa alitaka kupata ushauri kwanza kutoka kwa kaka yake hivyo bado anasubiriwa kufunguka zaidi. Endelea kufuatilia Magazeti ya Global Publishers.
WAUMINI WASUBIRIA TAMKO LA PENGO
Wakizungumza na gazeti hili juu ya sakata hilo, baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki mjini Moshi, walimuomba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo kulitolea tamko suala hilo ili kutuliza upepo na kumaliza ‘sintofahamu’ ya mustakabali wa Father Ngowi.
“Jambo hili ni zito na linalitia aibu kanisa na waumini wake. Tunaomba Kadinali Pengo atoe sauti ili tujue msimamo wa kanisa,” alisema Paulo Swai, mkazi wa mjini Moshi.
Hivi karibuni, Father Ngowi alikutwa na mkasa wa kudaiwa kufumaniwa akiwa kwenye nyumba yake parokiani, habari ambayo imekuwa gumzo kwa waumini wa Kanisa Katoliki nchini kote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment