http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Saturday, May 11, 2013

HUKUMU YA SHEHE PONDA

Richard Bukos na Makongoro Oging'
MAAJABU yamejitokeza kwenye hukumu iliyomkabili Katibu wa Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda na wenzake 49, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam juzi Alhamisi baada ya katibu huyo kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje na wengine kuachiwa huru.
...Akiwa Mahakamani akingoja hukumu yahe
SIRI YA KUPEWA KIFUNGO CHA NJE
Wakati wa utetezi wake mahakamani hapo baada ya kuingizwa hatiani na hakimu, Shehe Ponda kupitia wakili wake, Said Njama aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu amekaa gerezani kwa muda mrefu (tangu Oktoba, 2012).
Pili, Ponda alisema ni kesi yake ya kwanza kupatikana na hatia hivyo yeye si mtu tishio katika jamii.

WANAUME WALIA, WANAWAKE WACHEKA!!
Imezoeleka katika jamii nyingi wanawake ni viumbe dhaifu, wasioweza kuvumilia machungu na hivyo ni wepesi kumwaga machozi, lakini siku ya hukumu, wanaume walioachiwa huru ndiyo waliomwaga machozi bila kujizuia (angalia picha Uk.1).
Baadhi ya wanaume hao waliamua kupiga magoti na kuinua mikono juu huku wakilia kwa furaha ya kuwa huru.

Sasa, wakati hali ikiwa hivyo kwa wanaume hao, wanawake wao walishangilia ‘ushindi’ kwa vicheko vya furaha na kuonesha alama ya ushindi kwa kunyoosha ngumi juu, jambo lililowaacha vinywa wazi watu wengine na kuhoji iweje wanawake wacheke, wanaume walie?
Katika tukio hilo, wanawake ndiyo waliokuwa na kazi ngumu ya kuwabembeleza wanaume hao wasitishe kutoa machozi, jambo ambalo si kawaida kutokea.

WAGOMA KUONDOKA KIZIMBANI BAADA YA KUACHIWA HURU

Mara nyingi washitakiwa wanapoambiwa wako huru hutoka mkuku kizimbani wakati mwingine bila hata kugeuka, hali inayotafsiriwa kwamba huona kizimbani ni mahali penye nuksi, lakini washitakiwa hao walishangaza watu baada ya kuambiwa wako huru waondoke kizimbani lakini wao waliendelea kujiachia bila hofu wakisikiliza kesi ya Ponda ambaye alipatikana na hatia katika shitaka la pili ambalo ni kuingia kinguvu eneo lililokuwa likigombewa (Marcas).

HAKIMU ASOMA HUKUMU NA MSALABA SHINGONI

Maajabu ya tatu mahakamani hapo ni kitendo cha hakimu aliyekuwa akisoma hukumu hiyo, Agustina Mmbando kuvaa mkufu wenye msalaba ambao ulikuwa ukining’inia shingoni bila kujali kwamba ni rahisi watu kujua imani yake hasa kutokana na aina ya kesi.

SERIKALI ILIVYOJIPANGA

Baada ya kutangazwa kwa hukumu ya Ponda, vurugu na mayowe ya kushangilia vilitawala ndani na nje ya mahakama hiyo lakini askari zaidi ya 100 waliojikoki silaha za kutosha, yakiwemo mabomu, risasi za moto na maji ya kuwasha walikaa tayari kuwakabili.
Askari hao walikuwa katika magari aina ya Land Rover ‘Difenda’ zisizopungua 9, pikipiki 20 na farasi 2 walilizunguka kundi kubwa la watu lililoonekana kutaka kuchafua hali ya hewa na kulituliza.
Akiwa na kipaza sauti, afisa mmoja wa jeshi la polisi alilitaka kundi hilo kutawanyika kwa amani mahakamani hapo vinginevo jeshi hilo lingetumia nguvu ya ziada.

PONDA ASAINI FOMU, HAKIMU AMPA CHEO

Ponda alitakiwa kujaza fomu maalum zenye maelekezo ya hukumu yake huku hakimu akimtaka kwenda kuwa mlinzi wa amani na mtatuzi wa migogoro katika jumuiya yake.

MGOGORO WA ARDHI UPO PALEPALE

Licha ya hukumu hiyo, Hakimu Mmbando alisema kuhusu kesi ya mgogoro wa ardhi iliyokuwa ikimkabili Shehe Ponda, mahakama yake haina uwezo wa kusikiliza, hivyo akawashauri walalamikaji kama wanataka kuiendeleza waende Mahakama ya Ardhi.
Kesi iliyomtia hatiani ni shitaka la pili la kuvamia eneo la Marcas, Chang’ombe, jijini Dar kinyume na taratibu.

WAFUASI WATAKA KULISUKUMA GARI LA PONDA

Nje ya mahakama hiyo, wafuasi wa Ponda waliokuwa wakimsubiri walimshangilia baada ya kumwona na kutaka kulisukuma gari lake dogo aina ya Isuzu kama shujaa wa ‘milenia’ lakini dereva wake aliongeza kasi na kutokomea eneo hilo.

MAANDAMANO KUELEKEA MSIKITI WA MANYEMA

Pamoja na Ponda kutimua zake, wafuasi wake waliokosa nafasi ya kuongea nje baada ya kesi kumalizika, waliandamana wakisema wanakwenda Msikiti wa Manyema, Kariakoo, Dar kwa lengo la kuzungumza mawili matatu.

   SOURCE:::::::::: global publishers

No comments:

Post a Comment