HUKU sakata lake na Kituo cha Redio Clouds FM likiendelea kushika
kasi, habari ya mjini ni kwamba inadaiwa mwanamuziki Judith Wambura
Mbibo ‘Lady Jaydee’ leo anatarajia kufikishwa Mahakama ya Kinondoni, Dar
bila kutajwa aina ya mashitaka yanayomkabili.
Taarifa za mwanadada huyo kufikishwa mahakamani hapo, ziliibuka
chinichini kwenye mitandao ya kijamii, mwishoni mwa wiki iliyopita
ambapo baadaye Lady Jaydee alihoji kuwa pengine yeye ndiye anayestahili
‘kukinukisha’ kwa kuwapeleka mahakamani wasanii walio chini ya Tanzania
House of Talent (THT), Estarlina Sanga ‘Linah’ na Elias Barnaba ambao
anadai aliwalipa kianzio cha shoo yake ya Mei 31, mwaka huu kisha
kumchomolea dakika za mwisho.
“Hivi mahakamani sitakiwi kwenda mimi
ambaye wasanii wao wamechukua advance na kuafiki mbele ya camera na
wakanipa, It wasn’t me?” aliandika Lady Jaydee katika mtandao wa
Twitter.
KUMBUKUMBU
Kumbukumbu inaonesha, miongoni mwa maneno ambayo
yanadaiwa kuwa yaliuchafua uongozi wa Clouds ni yale ambayo Lady Jaydee
aliyaandika kupitia blogu yake hivi karibuni.
RUGE HAKUKAA KIMYA
Hata hivyo, siku chache baada ya Lady Jaydee
kuandika wosia huo mzito, Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti wa Clouds
Media Group, Ruge Mutahaba alitumia Kipindi cha Power Breakfast
kuzipangua hoja moja baada ya nyingine na mwishoni kumalizia kwa kusema
Jide anapaswa kusoma alama za nyakati kwani umri unakwenda na muziki
anapaswa kujipanga vizuri ili uweze kujimudu pindi zamu ya kushuka
kwenye gemu inapofika.
Ijumaa Wikienda ilifanya jitihada za kumtafuta
Lady Jaydee azungumzie kuhusiana na ishu ya kufikishwa kortini hiyo
lakini hakuweza kupatikana lakini kupitia akaunti yake ya mtandao wa
Twitter, alifafanua kauli hizo:
“Nimepata taarifa zisizo rasmi kuwa
nimefunguliwa kesi mahakamani, natumaini sitaitwa kizimbani tar. 31 May
ambayo ndiyo siku ya show.”
Baadaye aliongeza: “Ratiba ya usiku wa leo (Ijumaa) ni Machozi Band
kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu (leo) natakiwa Mahakama ya
Kinondoni. Taarifa zaidi zitafuata nikijua kinachoendelea. Ila kwa leo
mje tuburudike Nyumbani Lounge mpaka asubuhi.”
Hadi tunakwenda
mitamboni, mwanamuziki huyo anayetarajia kuzindua albamu yake ya Nothing
But The Truth, Mei 31, mwaka huu, alinukuliwa kuwa aliinadi shoo yake
ya kila wikiendi huku akibainisha kuwa anajiandaa kwenda mahakamani
Jumatatu (leo).
No comments:
Post a Comment