SPIKA wa Bunge Anne Makinda amelazimika kuahirisha shughuli za Bunge
mpaka jumatatu kwa lengo la kuinusuru Bajeti ya wizara ya maji baada ya
kuibuka malumbano makali baina ya serikali na wabunge huku wengi wao
wakionyesha dalili za wazi za kuipinga bajeti hiyo. Sanjari na
uamuzi huo Spika Makinda ameiagiza kamati ya Bajeti,kamati ya sekta na
Serikali kutafuta ufumbuzi wa nini kifanyike kabla ya kuruhusu mjadala
huo urudishwe Bungeni wiki ijayo kwa ajili ya majadiliano kabla ya
kupitishwa na wabunge. Spika Makinda anasema suala la maji
linawagusa watanzania kwa asilimia mia katika maisha yao ya kila siku na
kwamba kuendelea kujadili jambo linalopingwa na kila mbunge anayesimama
bila kujali itikadi za kisiasa Bunge litakuwa halitendi haki kwa jamii.
Awali Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliambia Bunge kuwa kutokana na
ufinyu wa bajeti ya maji kwa mwaka huu wa fedha serikali itatoa
kipaumbele kwa maeneo ya vijijini ambayo yanadaiwa kuwa katika hali
mbaya ya upatikanaji wa huduma hiyo. Waziri Mkuu Pinda ametoa kauli
hiyo kufuatia swali la Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman
Mbowe wakati wa maswali na majibu ya papo hapo ambayo huulizwa kwake na
wabunge kila siku ya alhamis. Katika swali lake Mbowe alitaka kujua
ni kwanini serikali isitoe kipaumbele kwenye suala la uvunaji wa maji
akiamini kuwa hatua hiyo inaweza kuwa suluhu mbadala ya kuondokana na
kero ya maji nchini. Wakichangia makadirio ya mapato na matumizi kwa
wizara ya maji baadhi ya wabunge wameitaka Serikali kutafuta njia
mbadala ya kumaliza changamoto ya huduma hiyo ambayo inadaiwa kutishia
usalama wa maisha kwa baadhi ya wanawake waishio vijijini ambapo wengi
wao hukumbana na wanyama hatari na hata nyoka nyakati za usiku.
Mapema jumatano hii akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya
wizara yake waziri wa maji Profesa Jumanne Maghembe amesema changamoto
kubwa inayoikabili sekta hiyo ni ongezeko la watu,ukuaji wa shughuli za
kiuchumi na kijamii pamoja na hujuma katika miundo mbinu ya maji
inayofanywa na baadhi ya watu wanaojihusisha na biashara ya vyuma
chakavu. Wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni
398.3 ambapo bilioni 18.9 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na
bilioni 379.4 ni fedha za maendeleo ingawa tarakimu hizo zinaweza
kubadilika wakati wowote kuanzia sasa baada ya majadiliano kati ya
kamati hizo mbili na serikali.
BAJETI YA MAJI YA KWAMA- TOMA MAONI JINA NA MAHALI

No comments:
Post a Comment