http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Thursday, September 28, 2017

Man United Yaandaa Paundi Milioni 88 Kumnasa Griezmann Baada Ya Costa Kutua Atletico

MANCHESTER, Uingereza- Manchester United wapo kwenye mchakato wa kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann kwa kitita cha paundi milioni 88 huku kocha Jose Mourinho akiwataka mabosi wa klabu hiyo kuhakikisha dili hilo linakamilika.
Tovuti ya The Express ya nchini Uingereza inaripoti kuwa Mourinho ameupa kipaumbele usajili wa mfaransa huyo mwishoni wa msimu baada ya kushuhudia akiikosa saini yake kwenye dirisha la usajili lililofungwa Septemba 1 mwaka huu.
Mourinho amekuwa na shauku kubwa ya usajili huo licha ya Atletico Madrid kufungiwa na FIFA kufanya usajili hadi Januari mwakani, lakini hata hivyo United wameendelea kufanya ushawishi huku wakitajwa kuweka paundi milioni 88 ambacho ni kiasi cha kumuuza mchezaji huyo kama ambavyo mkataba wake unahitaji
Matumaini ya kumsajili Griezmann kwa United yamekuwa makubwa hasa baada ya Atletico Madrid kukamilisha usajili wa Diego Costa kutoka Chelsea ambae atajiunga na kikosi hicho mwezi Januari mwakani
SOURCE

No comments:

Post a Comment