http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Sunday, June 15, 2014

MAREHEMU GEORGE TYSON AZIKWA HII LEO NCHINI KENYA

Hapa ndipo mwili wa Marehemu George Tyson ulipozikwa mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.George Tyson ambaye alikuwa ni mmoja wa Waongozaji filamu mahiri hapa nchini Tanzania,alifarika kwa ajali ya gari wakati akitokea mkoani Dodoma kikazi akirejea jijini Dar.Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.Amin.
Misa ya mwisho ya kumuombea marehemu George Tyson nyumbani kwao mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.
Ndugu na jamaa mbalimbali wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu George Tysombani kwako,katika kijiji cha Siaya nchini Kenya.
Baadhi ya Ndgu na Jamaa mbalimbali wakiwa kwenye maombolezo ya mwisho ya mazishi ya marehemu George Tyson mapema leo mchana,nyumbani kwao
Misa ya mwisho ya kumuombea marehemu George Tyson nyumbani kwao mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.
Mdau Felix akizungumza jambo na kuwashukuru Watanzania wote na wengineo walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kuhakikisha mpendwa wao,ambaye Mwenyezi Mungu kampenda zaida anaenda kuishi kwenye nyumba yake ya milele.
Watoto wa marehemu George Tyson wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwili wa aliyekuwa mwongoza filamu za Kibongo, marehemu George Otieno Okumu ‘Tyson’ (41) aliyefariki dunia Mei 30, mwaka huu kwa ajali mbaya ya gari nchini Tanzania na kusafirishwa kwao,Kenya umezikwa siku ya leo kijijini kwao Siaya  nchini Kenya.
 Mama wa Marehemu George Tyson, Mwongozaji Filam maarufu nchini Tanzania na Kenya akiweka udongo katika kaburi la mtoto wake, George Tyson .Chini ni mama wa marehemu akiwa na huzuni baada ya kuweka udongo katika kaburi la mwanae
 
 Mtoto wa Marehemu, Sonia akilia kwa uchungu wakati wa kuweka udongo katika kaburi la baba yake ....


Marehemu George Tyson katika  enzi  za  uhai  wake.

No comments:

Post a Comment