http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Sunday, August 18, 2013

YANGA YAICHAPA AZAM 1-0 NA KUTWAA NGAO YA JAMII


Kikosi cha Young Africans kilichoanza dhidi ya Azam FC
Young Africans imeendeleza wimbi la ushindi dhidi ya wana lamba lamba Azam FC kufuatia kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliofanyika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni ya leo.
Ukiwa ni mchezo nne kwa kocha Stewart Hall wa Azam FC  ndani ya mwaka mmoja, na mchezo wa tatu kwa kocha Ernie Brandts, Azam FC wameendelea kuteseka na jinamizi la kukutana na kichapo kila wanapokutana. 
Young Africana ambayo ilikua ikijufua katika viwanja vya shule ya Sekondari Loyola na kuweka kambi katika hosteli za klabu, imedhihirsha kuwa mafunzo ya kocha na mbinu ndio kitu kikubwa katika ushindi kufuatia Azam FC kuchezea kichapo huku ikiwa iliweka kambi nchini Afrika Kusini.
Iliwachukua dakika mbili tu watoto wa Jangwani kuhesabu bao la kwanza kupitia kwa kiungo Salum Telela aliyeukwamisha mpira wavuni akimalizia pasi safi ya mshambuliaji wa pembeni Saimon Msuva.
Mara baada ya bao hilo safi Yanga iliendelea kulishambulia lango la Azam FC lakini washambuliaji wake Jerson Tegete, Didier Kavumbagu hawakuwa makini na kupoteza nafasi za wazi katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Azam FC walifanya mashambulizi langoni mwa Yanga lakini mashuti ya Khamis Mcha, Kipre Tchetche hayakuwa na madhara kwa mlinda mlango Ally Mustapha 'Barthez' ambaye baadaye aliumia na kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Deogratius Munishi 'Dida'.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 1 - 0 Azam FC.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi timu zote zikisaka kujihakikishia ushindi huku Yanga ikimuingiza Hussein Javu kuchukua nafasi ya Jerson Tegete na Azam wakiwaingiza Gaudence Mwaikimba, Ibrahim Mwaipopo na Joackins Atudo wakichukua nafasi za John Bocco, Kipre Bolou na Erasto Nyoni.
Mabadiliko hayo hayakuzisaidia timu zote zaidi ya kuifanya Yanga iendelee kuulinda ushindi wake na mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 1- 0 Azam FC.
Kufuatia ushindi huo wa bao 1 - 0, Yanga imetwaa Ngao ya Hisani ambayo ilikabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sadick Mecky Sadik kwa nahodha wa timu Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Katika mchezo wa leo mlinzi Kelvin Yondani na mlinda mlango Ally Mustapha 'Barthez' walitolewa nje kufuatia kupata maumivu na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi zao kuchukuliwa na Mbuyu Twite na Deogratius Munishi.
Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez'/Deogratius Munishi 'Dida, 2.Juma Abdul, 3.David Kuhende, 4.Kelvin Yondani/Mbuyu Twite, 5.Nadir Haroub 'Cannavaro', 6.Athuman Idd 'Chuji, 7.Saimon Msuva, 8.Salum Telela, 9.Jerson Tegete/Hussein Javu, 10.Didier Kavumbagu, 11.Haruna Niyonzima
Azam FC: 1. Aishi Mnaula, 2.Erasto Nyoni/Joackins Atudo, 3.Wazir Salum, 4.David Mwantika, 5.Aggrey Morrsi, 6.Himid Mao, 7.Kipre Tchetche, 8.Salum Abubakar, 9.John Bocco/Gaudence Mwaikimba, 10.Michael Bolou/Ibrahim Mwaipopom, 11.Seif Karihe
Salum Telela (wa kwanza kulia) akishangilia bao alilowafunga Azam FC katika mchezo wa leo, anayemfuatia ni Saimon Msuva, Haruna Niyonzima na Jerson Tegete

No comments:

Post a Comment