MWENDESHA 
bodaboda mkazi wa kijiji cha Igalako wilayani Mbarali, Mbeya, Yohana 
Mkinga (17) ameuawa kwa kupigwa mapanga na kisha mwili wake kutelekezwa 
kwenye shamba la mpunga katika tukio linalohusishwa na wivu wa 
kimapenzi.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, 
Diwani Athumani amesema kuwa, mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha ya 
kukatwa mapanga, huku vidole viwili vya mkono wa kushoto vikiwa 
vimenyofolewa. Kamanda huyo ameongeza kuwa, jicho lake la kushoto la 
kijana huyo lilitobolewa na kutolewa. Aidha, mwili umekutwa na majeraha 
manne makubwa kichwani.
Alisema Mkinga ambaye aliondoka nyumbani kwake jioni ya Jumatano wiki
 hii akiwa na pikipiki aina ya Shinley yenye namba za usajili T770 BYH, 
mwili wake ulionekana siku mbili baadaye katika kijiji cha Muhela, 
Mbarali ambako pia pikipiki ilitelekezwa.
Aliongeza kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa, kijana huyo 
ameuawa kutokana na wivu wa mapenzi, akituhumiwa kuwa na uhusiano na mke
 wa Nicolaus Damson ambaye ametoweka baada ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa Kamanda Athumani, tayari mwili wa marehemu 
umeshakabidhiwa kwa ndugu huku juhudu za kuwasaka wahusika wa mauaji 
hayo zikiendelea.
Katika tukio jingine, Tegemeo Wilangali (29) ambaye ni mkulima wa 
kijiji cha Mwakaganda wilayani Mbarali, amekufa baada ya kukanyagwa na 
trekta alilokuwa analidandia likiwa katika mwendo kasi.
Kamanda Athumani amesema ajali hiyo ilitokea juzi kijijini hapo. 
Trekta hilo lenye namba za usajili T 885 BPY, likiwa na tela ambalo 
halina namba za usajili, lilikuwa likiendeshwa na Alex Kalonga (25), 
mkazi wa Ubaruku
 


 
No comments:
Post a Comment