JUMBA linalodaiwa kutumika kuendesha shughuli za ukahaba limebainika kuwapo katika eneo la Buguruni, jijini Dar es Salaam.
Uchunguzi
uliofanywa na Tanzania Daima, umebaini kuwapo kwa jumba ambalo
linatumika kama nyumba ya kulala wageni, ambako idadi kubwa ya makahaba
hujazana na kuendesha biashara ya kuuza miili yao bila
wasiwasi.
Wasichana wanaofanya biashara hizo hutoza kiasi cha sh 5,000
kama huduma ya ngono na chumba kwa matumizi ya muda mfupi.
Biashara hiyo ambayo imeleta usumbufu mkubwa kwa wakazi wengi wanaopakana na nyumba hiyo, imekuwa
ikifanikiwa kutokana na kuwapo kwa baadhi ya askari polisi wanaodaiwa kuwalinda wasichana hao pamoja na mmiliki wa nyumba hiyo.
Nyumba
hiyo inavyo vyumba vingi vinavyotozwa kiasi sha sh 1,200 kwa chumba
pamoja na kondomu. Kadhalika wasichana wenye umri wa miaka 15, ni
miongoni mwa wanaofanya biashara hiyo.
Mjumbe wa serikali ya mtaa
wa eneo hilo, Amiri Banza, alikiri kuwapo kwa biashara hiyo, ingawa
alisema wamejaribu sana kuzuia hali hiyo bila mafanikio:
“Tumechoka na
hii kadhia, tumeripoti kwa viongozi wa Kata hadi polisi lakini hakuna
hatua yoyote iliyochukuliwa. Kama wakija polisi wanawakamata, halafu
wanawaachia,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa
Ilala, Marietha Minangi alipoulizwa juu ya kuwapo kwa jumba hilo alisema
hajui chochote.: “Mimi sijapata taarifa hizo na ndiyo kwanza
ninakusikia wewe,” alisema.
Alipoulizwa kuhusu polisi kufika
kwenye jumba hilo na kuchukua rushwa na kuondoka alisema: “Sina
ushahidi, kama wapo polisi wanafanya hivyo ni kosa,” alisema Minangi na
kuongeza kuwa polisi wanafanya doria maeneo hayo na mara kadhaa
wamewakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha
mahakamani.
No comments:
Post a Comment