http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Saturday, April 27, 2013

TFF yaikata YANGA kwenye mapato yake kwa ajili ya MBUYU TWITE na YANGA waziria fedha nyingin


IMEFAHAMIKA kuwa Klabu ya Yanga, imesusia mgawo wa mapato ya milangoni katika mechi zao za hivi karibuni za Ligi Kuu Bara kutoka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa sababu inayoelezwa kuwepo na makato ya deni la beki wao, Mbuyu Twite.
TFF ilifikia hatua hiyo kutokana na deni linalodaiwa kuwa milioni 50 wanalodaiwa na Simba ambalo lilitokana na sakata la usajili wa Mbuyu aliyepokea fedha za Simba kisha kusaini Yanga.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameliambia Championi Ijumaa kuwa, mgawo wa fedha walizozigomea ni dhidi ya JKT Ruvu iliyoingiza shilingi milioni 66, Azam milioni 24 na nyingine dhidi ya African Lyon.
Mwalusako alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kugundua fedha zao kukatwa bila ya kuwepo makubaliano kati yao, Simba na TFF.
“Tumeamua kuwaachia kabisa fedha za mechi tatu tulizocheza ambazo dhidi ya Lyon, Azam na JKT Ruvu, baada ya kugundua kuwa TFF inakata fedha zetu kwenye deni la Twite na kuzipeleka Simba, kitu ambacho siyo sahihi isitoshe shirikisho lilithibitisha usajili wa beki huyo kuwa tulikuwa sahihi iweje hivi sasa wakate mapato yetu!
“Deni hilo sisi halituhusu, kama Simba wangekuwa wanataka fedha zao walizotumia kumsajili wangechukua walipoletewa na Lupopo iliyomsajili, hivyo sisi tunasisitiza fedha hatutazipokea hadi zitakapokuwa kamili,” alisema Mwalusako.


No comments:

Post a Comment