UWANJA maarufu wa Brazil, Maracana Stadium umefunguliwa tena jana usiku baada ya miaka mitatu ya ukarabati, na upo tayari kwa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 na sherehe za ufunguzi za Olimpiki ya mwaka 2016.
Mchezo wa kwanza kufanyika kwenye Uwanja
huo baada ya kukamilika kwa ukarabati wake uliikutanihsa timu ya
Marafiki wa wa Ronaldo dhidi ya Marafiki wa Bebeto jana.
Rais wa Brazil, Dilma Rousseff, rais wa
zamani, Luiz Inacio Lula da Silva na watu wengine wenye majina makubwa
waliokuwa miongoni mwa watu 30,000 waliohudhuria ufunguzi huo.
Washington, mshambuliaji wa zamani wa
Fluminense, alifunga bao la kwanza jana kwa kichwa dakika ya 16, wakati
Ronaldo, ambaye enzi zake anacheza hakuwa kufunga kabisa kwenye Uwanja
huo, jana alifunga bao lingine.
Maracana ulikuwa mmoja wa viwanja
vikubwa duniani, wakati watu 200,000 waliposhuhudia Fainali ya Kombe la
Dunia mwaka 1950 kati ya Brazil na Uruguay. Pia ni uwanja ambao, Pele
alifunga bao lake la 1,000 mwaka1969.
'Sinagogi la Soka': Ukarabati
umekamilika Uwanja wa Maracana uliopo Rio de Janeiro, Brazil na
umefunguliwa jana kwa magwiji wa soka Brazil, wakiongozwa na Ronaldo na
Bebeto kucheza baina yao.
Heshima: Welder Antonio Pereira aliungana na gwiji wa Brazil, Ronaldo katika sherehe za ufunguzi
Bao la kwanza: Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Washington alifunga bao la kwanza jana katika Maracana mpya
Busu la uepndo: Washington akibusu nyasi za Uwanja huo
Mamia kadhaa walikandia zoezi hilo kwa
njia ya amani, wakibeba mabango ya kubeza kwamba Serikali ya nchi hiyo
itapata hasara katika uwekezaji wake huo
Timbwili: Polisi wakiwakamata watu waliokuwa wakifanya vurugu nje ya Uwanja wa Maracana Ijumaa
Welder Antonio Pereira alipewa heshima ya kwenda kumpasia mpira Ronaldo kuanzisha mchezo huo wa sherehe za ufunguzi.
Ronaldo, ambaye aliiwezesha Brazil
kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1994 na 2002, pia ni Mjumbe wa Kamati ya
Maandalizi ya Fainali zijazo za Kombe la Dunia
Gwiji: Mshindi wa fainali mbili za Kombe
la Dunia, Ronaldo akiupungia umati jana. Enzi zake anacheza soka
hakuwaghi kufunga bao Uwanja wa Maracana
Bado anaweza: Ronaldo, aliyeifungia Brazil mabao 62 katika mechi 98, akipokea pasi jana
Anakumbushia: Ronaldo akipasua...
Mkongwe: Bebeto, ambaye alikuwa Nahodha wa timu nyingine, akimtoka mchezaji jana
Anakwenda na mpira: Mkongwe wa Brazil, Junior, ambaye aliichezea Brazil mechi 70, akiambaa na mpira jana
No comments:
Post a Comment