MMILIKI wa Manchester City, Sheikh Mansour wa Abu Dhabi yupo karibuni kuwekeza kiasi cha dola za Kimarekani, Milioni 100 kuanzisha timu mpya itakayoshiriki katika Ligi Kuu ya Marekani, ijulikanayo kama Major League Soccer ambayo itakuwa na maskani New York.
mauthaman.blogspot.com inafahamu
dili hilo limekaa vizuri kufanikisha na Sheikh ana matumaini yeye na
Maofisa wa MLS, watakuwa kwenye nafasi ya kutangaza mpango huo wakati
kikosi cha Roberto Mancini kitakapokwenda Marekani kucheza na Chelsea
Jijini New York katika mchezo maalum wa hisani mwishoni mwa mwezi ujao.
Malengo mapya: Sheikh Mansour (katikati) anataka kuwekeza MLS dola Milioni 100
Wakali zaidi wataungana naye: Thierry Henry tayari anacheza New York Red Bulls
No comments:
Post a Comment