Manji akimkabidhi Ridhiwani hati ya jengo la Mafia lililopo mtaa wa Livingstone, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Manji akiongea na wanachama wa Yanga pamoja na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Ridhiwani Kikwete na Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako (kushoto).
Mwenyekiti wa Ujenzi wa Jengo la Mafia, Ridhiwani Kikwete, akiongea na wanachama wa Yanga pamoja na wanahabari (hawapo pichani).
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji, amemtangaza Ridhiwani Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Ujenzi wa Jengo lao la Mafia lililopo mtaa wa Livingstone, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo iliyopo Jangwani Dar es Salaam, Manji alisema anaamini taaluma ya uanasheria aliyonayo itasaidia kusimamia jengo hilo kwa kusaidiana na wahandisi.
Manji alisema, kamati hiyo tayari imeanza kazi yake ya ujenzi huo na tayari imewapa notisi wafanyabiashra waliopo kwenye jengo hilo linalomilikiwa na Yanga.
Alisema, mwenyekiti huyo wamempa jukumu la kuwachagua wajumbe wake atakaofanya nao kazi bila ya kuingiliwa na mtu yeyote.
No comments:
Post a Comment