KOCHA David Moyes anakaribia kushinda
vita yake ya kuwania saini za wachezaji wa Everton, Leighton Baines na
Marouane Fellaini baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba, klabu yake ya
zamani iko tayari kuwauza nyota wake hao.
Everton imekuwa ikilalama dhidi ya Moyes
na Manchester United tangu ikatae ofa ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya
England ya Pauni Milioni 28 kwa ajili ya nyota hao wawili wa Goodison
Park.
Wamekubaliana na ofa hiyo na kocha wa Everton, Roberto Martinez ameisifu United imekuwa na tabia nzuri.
Nakuja kwako: David Moyes anakaribia kuwanasa wachezaji wake wa zamani Leighton Baines na Marouane Fellaini
Anaonekana vizuri: Baines akiwa mazoezini na Everton
Anabaki au anaondoka? Fellaini (kulia) na Baines mazoezini na Everton kujiandaa na mchezo dhidi ya West Brom
No comments:
Post a Comment