Timu ya Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa Ligu Kuu ya Vodacom nchini VPL kwa kuwa na point 39 kesho itashuka dimbani kupamabana na timu ya Kagera Sugar kutoka mjini Bukoba, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam majira ya saa 10 jioni.
Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kimefanya mazoezi ya
asubuhi katika uwanja wa mabatini kijitonyma ikiwa ni mazoezi ya mwisho
kabla ya mchezo huo ambao utafanyika kesho katika Uwanja wa Taifa
kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Baada
ya kuichapa Azam FC kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika mwishoni mwa
juma na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom,
Young Africans itashuka dimbani kuhakikisha inaibuka na pointi 3 muhimu
ili kuendelea kuongoza msimamo huo wa VPL.
Mara
baada ya mazoezi kocha Brandts amesema kikosi chake kipo katika hali
nzuri kuelekea mchezo huo wa kesho, na hakuna mchezaji aliye majeruhi ,
hivyo wachezaji wake wote wapo tayari kabisa kuwakabili wakata miwa wa
Kagera Sugar na kuhakikisha wanaibuka na pointi 3 muhimu.
Aidha
wapenzi, washabiki na wanachama wa klabu ya Yanga mnaombwa kujitokeza
kwa wingi katika mchezo wa kesho, kuja kuwapa sapoti wachezaji,
kuwashangilia tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho wa mchezo, kwani
mashabikinni sialaha kubwa katika kuisaidia timu kuweza kufanya vizuri.
Kuelekea
mchezo wa kesho, timu imendelea kuwa kambini katika Hoteli ya Tansoma
ambapo iliingia tangu jana asubuhi mara baada ya mazoezi na itaendelea
kuwa hapo mpaka siku ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar.
Viingilio vya mchezo wa kesho ni:
VIP A Tshs 20,000/=
VIP B & C Tshs 15,000/=
Orange Tshs 8,000/=
Blue & Green Tshs 5,000/=
No comments:
Post a Comment