Mechi Ya Yanga, Azam Yaingiza Mil. 240/- |
Mechi
namba 120 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 23 mwaka
huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga
kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam imeingiza sh. 239,686,000.
Watazamaji
39,315 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata
mgawo wa sh. 58,794,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyolipwa ni sh. 36,562,271.19.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata
tiketi hizo walikuwa 33,315 na kuingiza sh. 165,655,000 wakati idadi
ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia
washabiki 485 na kuingiza sh. 9,700,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 29,895,725.82,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 17,937,435.49, Kamati ya Ligi
sh. 17,937,435.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
8,968,717.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 6,975,669.36.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
|
No comments:
Post a Comment