KIKOSI
cha wachezaji 18 wa timu ya soka ya Simba kinatarajiwa kuondoka
Alfajiri ya kesho kwenda Luanda, Angola tayari kwa mechi yao ya
marudiano ya ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Recreativo do
Libolo ya huko utakaopigwa keshokutwa katika mji wa Caculo.
Awali mchezo huo ilikuwa upigwe kesho mjini Luanda kabla ya kusogezwa hadi keshokutwa ambapo sasa utapigwa katika mji wa Caculo.
Akizungumza
mjini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga
amesema kwamba msafara wa timu hiyo utakaokuwa chini ya mjumbe wa kamati
ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Mohsin Balhabou
utaondoka kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ).
Aliwataja
wachezaji walioondoka ni pamoja na Juma Kaseja, Abbel Dhaira, Nassor
Said ‘Chollo’, Amir Maftah, Juma Nyosso, Shomari Kapombe, Komabil Keita,
Salim Kinje, Kiggi Makassy, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Haruna Moshi
‘Boban’, Mrisho Ngassa, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Abdallah Seseme,
Haruna Chanongo na Abdallah Juma.
Aidha,
Kamwaga aliwataja viongozi watakaoambatana na timu ni pamoja na
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharia Hans Poppe, kocha Mkuu Mfaransa
Patrick Liewig, kocha msaidizi Jamhuri kihwelo ‘Julio’ , Kocha wa
makipa James Kisaka, Meneja Mosse Basena, Daktari Cossmas Kapinga na
Mtunza vifaa, Kessy.
Kamwaga
alisema kocha mkuu wa timu hiyo, Liewing amekifanyia kazi kikosi chake
kwa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa awali, hivyo
wana uhakika wa kuibukaa na ushindi ugenini.
Simba
ambayo ilifungwa bao 1-0 katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya
Kwanza, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Recreativo de Libolo, inahitaji
kushinda 2-0 ili isonge mbele.
No comments:
Post a Comment