#1 Floyd Mayweather
Total earnings: $85 million
#2 Manny Pacquiao
Total earnings: $62 million
#3 Tiger Woods
Total earnings: $59.4 million
#4 LeBron James
Total earnings: $53 million
#5 Roger Federer
Total earnings: $52.7 million
#6 Kobe Bryant
Total earnings: $52.3 million
#7 Phil Mickelson
Total earnings: $47.8 million
#8 David Beckham
Total earnings: $46 million
#9 Cristiano Ronaldo
Total earnings: $42.5 million
#10 Peyton Manning
Total earnings: $42.4 million
*******************************************************
#11 Lionel Messi
Total earnings: $39 million
Total earnings: $85 million
#2 Manny Pacquiao
Total earnings: $62 million
#3 Tiger Woods
Total earnings: $59.4 million
#4 LeBron James
Total earnings: $53 million
#5 Roger Federer
Total earnings: $52.7 million
#6 Kobe Bryant
Total earnings: $52.3 million
#7 Phil Mickelson
Total earnings: $47.8 million
#8 David Beckham
Total earnings: $46 million
#9 Cristiano Ronaldo
Total earnings: $42.5 million
#10 Peyton Manning
Total earnings: $42.4 million
*******************************************************
#11 Lionel Messi
Total earnings: $39 million
MANCHESTER UNITED YAONGOZA TENA KWA TIMU YA MICHEZO YENYE THAMANI KUBWA ZAIDI DUNIANI
Jarida
maarufu la kimarekani la Forbes leo hii limetoa tena listi ya vilabu
vya michezo yote vyenye thamani kubwa duniani, na kwa mara nyingine tena
pamoja na kutochukua kombe lolote msimu uliopita na kutolewa mapema
kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya Manchester United imeendelea kushika
usukani mwa vilabu tajiri duniani huku ikifuatiwa na Real Madrid.
Timu
nyingine za mchezo wa soka zilizopo kwenye Top 10 ni Barcelona
wanaoshika nafasi ya nane, huku Arsenal ya England ambayo haijchukua
kombe lolote kwa miaka inayokaribia kufikia nane ikishika nafasi ya 10,
wakiwazidi mabingwa wapya wa Ulaya Chelsea wanaoshika nafasi ya 45 huku
matajiri wa England Man City wakiwa hawapo hata kwenye Top 50. Timu
nyingine za soka zilizopo kwenye listi hiyo ni Bayern Munich wanashika
nafasi ya 11, AC Milan wanashika nafasi ya 27.
#1 Manchester United ($2.23 billion)
#3 New York Yankees ($1.85 billion)
#5 Washington Redskins ($1.56 billion)
#6 New England Patriots ($1.4 billion)
#9 New York Giants ($1.3 billion)
RASHID MATUMLA AENDELEA KUPOKEA VIPIGO - ADUNDWA KWA TKO HUKO UJERUMANI
Bondia Benjamin Simon wa Ujerumani akipozi na Rashid Matumla 'Snake Man' wa Tanzania kabla ya pambano lao lililofanyika Jumamosi usiku. |
BONDIA gwiji nchini Tanzania, Rashid Matumla 'Snake Man' amepigwa kwa Technical Knock-out ya raundi ya nne dhidi ya bondia Benjamin Simon wa Ujerumani katika pambano lao la uzani wa Supermiddle lililokuwa kuwania mkanda wa IBF kwenye Ukumbi wa Universal, Ujerumani usiku wa kuamkia Jumapili.
Pambano hilo la raundi 12 lilikuwa ni la pili baina ya mabondia hao baada ya Matumla kupigwa kwa pointi katika pambano lao la awali lililofanyika Februari 6, 2010 Boxtempel, Ujerumani.
Mratibu wa pambano hilo, Ali Bakari 'Champion' wa Champion Sports Promotions ya Buguruni jijini Dar es Salaam akishirikiana na African Camp Promotion ya Kenya chini ya mkurugenzi wake, Thomas Mutua, alisema kuwa Matumla atarejea leo kupitia Nairobi.
Matumla aliondoka nchini Julai 10 kwa kupitia Nairobi, Kenya kwa ajili ya pambano hilo la usiku wa Jumamosi Julai 14.
source:straikamkali.blogspot.com
DOMAYO NA SINGANO 'MESSI' WASHINDWA KUIEPUSHA NGONGORO HEROES NA KIPIGO CHA PILI KUTOKA KWA RWANDA
TIMU ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, Ngorongoro Heroes, jana kwa mara ya pili ilishindwa kutamba mbele ya vijana wenzao wa Rwanda baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo wao kwanza Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya jiji, Heroes pia ilichapwa mabao 2-0.
Timu ya Rwanda |
Vijana hao wa Tanzania wanajiandaa kwa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika kwa Vijana mwaka 2013 dhidi ya Nigeria baadaye mwezi huu.
Vijana wa Rwanda walikuwa wa kwanza kulifikia lango la Ngorongoro na kujipatia bao la kuongoza dakika ya pili kupitia kwa Nsimiyiman Imran aliyeunganisha wavuni pasi ya Kabanda Boifil.
Heroes ikiwa na Frank Domayo, Omega Same, Saimon Msuva na Ramadhan Singano walitawala kwa kiasi kikubwa sehemu ya kiungo.
Ikicheza mbele ya mashabiki wachache waliojitokeza uwanjani, Heroes ilisawazisha bao hilo dakika ya 30 kwa mkwaju wa penalti uliosababishwa na Umwengeri Patrick kumchezea vibaya Singano.
Kiki hiyo ya penalti ilikwamishwa vizuri kwenye kamba na mchezaji Atepele Green na kuzifanya timu hizo kumaliza nusu ya kwanza zikitoshana nguvu ya bao 1-1.
Vijana wa Rwanda, kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza kufunga bao la haraka, ndivyo walivyofanya kipindi cha pili ambapo iliwachukua dakika nane kufunga bao la pili.
Bao hilo lilifungwa na Nsimiyimana Imran aliyetumia vizuri fursa kuchelewa kujipanga kwa mabeki wa Heroes na kuujaza mpira wavuni akimalizia pasi ya Tibingana Charles.
Baada ya bao hilo, Rwanda walichukuwa utawala wa mchezo na kufanya mashambulizi jinsi walivyotaka kwenye lango la Heroes.
Wenyeji walizinduka katika dakika ya 71 baada ya kufanya shambulizi kubwa langoni mwa Rwanda lililoishia kwa shuti kali la Domayo kupanguliwa na mlinda mlango Rafael Stevin.
Kocha Msaidizi wa Heroes, Adolph Richard alikiri kipigo hico, lakini akasema kimewapa mazoezi ya kutosha na kufanya marekebisho kabla ya mcehzo dhidi ya Nigeria.
News courtesy of Mwananchi.co.tz
DERRICK WALULYA AGEUKA LULU KWA MASHABIKI WA SIMBA
Baada ya jana kucheza kwa kiwango cha juu kwenye mchezo kati ya timu yake ya zamani na sasa, URA vs Simba, baadhi ya mashabiki wa Simba wamesema beki huyo aliondolewa Simba kimajungu na alikuwa hapangwi kwa sababu ya makocha kuangalia majina sio viwango.
HARUNA NIYONZIMA: MASHABIKI MSIHOFU TUTALIBAKISHA KOMBE JANGWANI
KIUNGO
wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima ameondoa hofu mashabiki wa timu
hiyo katika kutetea Ubingwa wao wanaoushikilia wa Kombe la Kagame
walilolichukua 2011.
Yanga
jana walianza vibaya kutetea ubingwa huo baada ya kufungwa na wapinzani
wao Atletico mabao 2-0, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.
Niyonzima
alisema, bado wananafasi kubwa ya kulibakisha kombe hilo la Kagame
kutokana na uimara wa kikosi chake, mashabiki wanachotakiwa ni kuendelea
kuwasapoti ili mechi zinafuata washinde.
Kiungo huyo raia wa Rwanda alisema, anaamini Kocha wao Mkuu,
Tom Saintfiet ameyaona mapungufu atakayoyafanyia kabla ya mechi
inayofuata dhidi ya Wau Salaam itakayochezwa Jumanne ijayo saa 10:00
jioni katika Uwanja wa Taifa.
Mrwanda huyo, kipigo walichokipata dhidi
ya Atletico ni cha bahati mbaya, badala yake watajipanga kwa kushinda
kila mechi watakayokutana nayo ili wafanikishe malengo yao.
mwisho
TIKETI ZA ELETRONIKI: CRDB YASHINDA TENDA YA KUTENGENEZA TIKETI ZA KUINGILIA UWANJANI
Benki
ya CRDB PLC imeibuka mshindi wa tenda ya kutengeneza tiketi za
elektroniki za kuingilia uwanjani iliyotangazwa na Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF).
Kampuni
saba zilijitokeza katika hatua ya awali ya kuonesha nia (Expression of
Interest) kwa ajili ya tenda hiyo ambapo Aprili 19 mwaka huu Kamati ya
Mipango na Fedha ya TFF ambayo ndiyo Bodi ya Tenda ya shirikisho
ilipitia maombi hayo na kupitisha nne kati ya hizo.
Baadaye
kampuni hizo nne; CRDB Bank PLC, Prime Time Promotions, Punchlines (T)
Limited na SKIDATA People Access Inc. zilitakiwa kuwasilisha rasmi
tenda zao zikionesha jinsi zitakavyofanya shughuli hiyo pamoja na
gharama ya utengenezaji kwa tiketi moja.
Bodi
ya Tenda ya TFF ilikutana Julai 13 mwaka huu kwa ajili ya kupitia
tenda hizo ambapo kampuni zote nne zilifanya uwasilishaji
(presentation) wa jinsi zitakavyofanya shughuli hiyo, na baadaye kuipa
kazi hiyo benki ya CRDB.
Uamuzi
huo wa Bodi ya Tenda uliwasilishwa mbele ya Kamati ya Utendaji ya TFF.
Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake kilichofanyika Julai 14
mwaka huu iliridhia uteuzi huo wa benki ya CRDB.
Baadhi
ya vigezo ambavyo Bodi ya Tenda ya TFF iliangalia na kuipa CRDB tenda
ni uwezo wa kufanya kazi hiyo (capacity), hadhi yake mbele ya jamii
(credibility) katika shughuli inazofanya na teknolojia ya kisasa
itakayotumika kutengeneza tiketi hizo.
Uamuzi
wa TFF kutangaza tenda hizo ulilenga kuimarisha udhibiti wa mapato ya
milangoni na kurahisisha mtiririko mzima wa washabiki kupata tiketi na
kuingia viwanjani.
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga amesema: “Hatua hii ni muhimu sana, kwani
tulikuwa tukiisubiri kwa muda mrefu. Si tu itaimarisha udhibiti wa
mapato, bali pia itaondoa matatizo ya tiketi na kuendelea kujenga
credibility (kuaminika) ya TFF. Mafanikio haya si kwa TFF pekee bali
mpira wa miguu kwa ujumla.”
Sunday, July 15, 2012
YUSUPH MANJI NDIO BOSI MPYA WA YANGA - ASHINDA KWA ASILIMIA 97. SANGA MSAIDIZI WAKE.
Kwa mujibu wa tovuti ya klabu ya Yanga haya ndio matokeo kamili ya wagombea ni:
Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876) 97.0%, John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%
Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)
kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama
SAKATA LA USAJILI WA YONDANI: SIMBA YAIANDIKIA BARUA KALI TFF KWA SABABU YA KELVIN YONDAN
Simba Sports Club imesikitishwa na hatua ya Katibu Mkuu wa TFF kujichukulia mamlaka ya Kamati ya Katiba na Sheria na kuamua mustakabari wa suala la Kelvin Yondani kwa barua yenye kumb namba TFF/TECH/GC.12/62 ikijibu pingamizi la Simba Sports Club lililokuwa likitaka mgogoro huo uamuliwe na chombo husika.
Masikitiko hayo ya Simba Sports Club yanatokana na jinsi haki na misingi bora ya uendeshaji wa mpira inavyoonekana kupindishwa waziwazi kwani Simba Sports Club imeshaandika barua nyingine mbili kwa Rais Tenga moja ya terehe 7/6/2012 yenye Kumb na SSC/5/6/02 ikilalamika juu ya uendeshwaji wa sakata zima la udanganyifu wa usajili wa mchezaji wa Simba Kelvin Yondani ambayo Rais alitoa maagizo kwa Katibu Mkuu na nakala kuja kwa Simba SC kwa barua pepe ya tarehe 8/6/2012 lakini baada ya kutofanyika utekelezaji wowote na badala yake watendaji wa TFF kuendelea kuongea katika vyombo vya habari wakisema mchezaji huyo ni mchezaji huru, Simba Sports Club iliandika barua nyingine kwa Rais Tenga juu ya kukosa imani na sekretarieti ya TFF kwa barua ya tarehe 23/6/2012 yenye kumb na. SSC/24/6/02 jambo ambalo limeonekana wazi kwamba sekretarieti ya TFF haitendi haki kwa Simba kwa jinsi ambavyo haikufanyia kazi barua mbili lakini Katibu Mkuu wa TFF amekuwa mwepesi wa kujibu pingamizi wakati si kazi yake ili mradi timu yake ya Yanga mabayo yeye ni mwanachama ifanikiwe jambo lake.
Katika barua ya pingamizi dhidi ya mchezaji Kelvin Yondani kutumiwa na klabu ya Yanga katika michezo ya kirafiki na ile ya CECAFA ya tarehe 11/7/2012 yenye kumb namba SSC/1/7/02 Simba Sports Club iliomba suala la mchezaji huyo lipelekwe katika kikao cha kamati ya katiba na sheria ambayo muda wake wa kukaa bado kwani kamati hiyo inaweza kukaa baada ya wiki mbili za kufunga usajili na kupokea pingamizi mbalimbali lakini taarifa za uhakika ni kwamba kamati hiyo ilijaribu kuitishwa haraka haraka ili kulitolea suala hili uamuzi lakini corum haikutimia hivyo ikashindwa kutoa maamuzi lakini kwa ubabe Katibu Mkuu akaamua kujichukulia mamlaka yasiyokuwa yake na kumpa leseni ya Yanga Kelvin Yondani huku Simba ikipokea majibu tarehe 14/7/2012 kwa barua uwanja wa Taifa wakati mechi kati ya Yanga na Atletico imeshaanza na ipo dakika ya 18.
Katika barua yake ya kumuidhinisha Kelvin Yondani katibu mkuu kakiri kuwepo kwa mkataba wa Yondani na Simba unaoisha mei 31, 2012 na kakiri pia kupokea nyaraka ya makubaliano ya Simba SC na Kelvin Yondani lakini kwa sababu yeye si mwanasheria na ndio maana kazi hiyo ni ya kamati ya katiba na sheria amezitafsilia pande mbili za mkataba yaani Simba Sports Club na Kelvin Yondani nia yao wakati wanaingia mkataba kwamba mkataba utaanza tarehe 23 december 2012 na kuweka kiambatanisho cha sehemu ya kusaini ya Simba Sports Club ambayo kwa sababu za kibinadamu ilikosewa na inasomeka tarehe 23 december 2012.
Katibu Mkuu wa TFF ameshindwa/amejikataza kuusoma mkataba tangu mwanzo na kuona nia za pande za mkataba ni zipi kwani katika ukurasa wa kwanza mkataba unasoma kwamba umesainiwa tarehe 23/12/2011, pia mkataba unatambua uwepo wa mkataba wa pande hizo mbili unaoisha tarehe 31/5/2012 na pande husika katika mkataba zimeonyesha nia ya kuongeza mkataba mara tu ule wa awali unapoisha.
Katika kipengele cha kwanza mkataba umeshuhudia pande zikitamka waziwazi kwamba mkataba umeongezwa kuanzia (effective) tarehe 1/6/2012 mara tu mkataba wa awali unapoisha sasa inashangaza Katibu Mkuu anazitafsiria pande nia zao kwamba mkataba utaanza tarehe 23/12/2012 wakati mkataba umetamka waziwazi.
Pia sehemu aliposaini mchezaji Kelvin Yondani imeonyeshwa waziwazi kwamba kasaini tarehe 23/12/2011 hivyo kuacha hitimisho lisilo na shaka kwamba Katibu Mkuu wa TFF amekiuka na kujivika mamlaka yasiyo yake ili kutekeleza unazi wake wa Yanga.
Simba Sports Club inakusudia kuyakatia rufaa maamuzi haya ya Katibu Mkuu wa TFF na ipo tayari kufuata mikondo yote ya sheria mpaka haki ipatikane kwani itatumia taasisi za TFF kwanza na isiporidhishwa na maamuzi itapeleka suala hili CAF mpaka FIFA na jambo la kushukuru ni kwamba Shirikisho la TFF limeanza kujibu barua za Simba SC suala ambalo linaanza kutoa mwanga wa nia ya kutotenda haki lakini barua hizo zitasaidia kuwaonyesha watu wa nje kama tukifika huko jinsi mpira wa Tanzania unavyoendeshwa kinazi na viongozi wa Shirikisho.
Imetolewa na
Simba Sports Club
VIELELEZO VYA SIMBA
Kusoma vizuri double click |
KIBONZO CHA LEO: SIMBA NA YANGA ZIKITOLEWA MAPEMA KAGAME ITAISHIA KATI KWA HALI HII
Mapato yaliyopatikana kwenye uwanja wa Chamazi Complex kwa mechi mbili za Kagame |
Breaking news! Abdallah Bin Kleb,Aaron Nyanda na Moses Katabalo washinda !
Taarifa nilizozipata hivi punde,wagombea watatu kwenye nafasi za ujumbe
Abdallah Bin Kleb,Aaron Nyanda na Moses Katabalo wamechaguliwa kwa
kishindo kuwa wajumbe kwenye uchaguzi mdogo wa wa Klabu ya Yanga
uliofanyika hii leo.
Yusuf Manji na Clement Sanga so far so good!
Taarifa nilizozipata hivi punde kutoka ndani ya ukumbi wa Diamond
Jubilee wagombea wawili kwenye uchaguzi wa Yanga bwana Yusuf Manji
anayegombea nafasi ya uenyekiti pamoja na bwana Clement Sanga anayewania
nafasi ya umakamu mwenyekiti wanaongoza kwa mbali.taarifa zaidi
zitakuja!
BAADA YA KULWA(YANGA) KUPIGWA 2-0: DOTO(SIMBA) NAE LEO ANYOLEWA 2-0 NA URA
Derrick Walulya mchezaji wa timu ya URA FC kutoka nchini Uganda ambaye
aliwahi kuchezea timu ya Simba pia ya Tanzania akimiliki mpira mbele
ya Felix Sunzu mshabuliaji wa timu ya Simba katika mchezo wa kuwania
kombe la Kagame linaloandaliwa na Shirikisho la Vyama vya michezo
Afrika Mashariki CECAFA unaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jioni hii
mpaka sasa mpira umekwisha na timu ya URA imeifunga timu ya Simba
magoli 2-0. magoli hayo yamefungwa na mchezaji Feni Ali wa URA FC.
Waamuzi wakiongoza timu kuingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo.
Wachezaji
wa timu za Simba ya Tanzania na URA ya Uganda wakisalimiana kabla ya
kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Watangazaji wa kituo cha televisheni cha Supersport cha Afrika Kusini
wakitoa tathmini ya mchezo huo kabla ya timu hizo kukutana ambapo
inaonyesha kuwa Simba mara nyingi imekuwa ikifungwa na URA FC wakati
timu hizo zinapokutana katika michuano mbalimbali.
Mashabiki
wa timu ya Simba wakiwa wamefurika katika uwanja wa Taifa kujionea timu
yao ikicheza na Waganda URA FC. (Picha kwa hisani ya
fullshangwe.blogspot.com)
MANCHESTER UNITED NDIO MABINGWA WA SERENGETI FIESTA BONANZA DSM
Mashabiki wa Manchester United wakishangilia kwa nguvu baada ya kukabidhiwa kombe lao. |
Mashabiki wa Manchester United wakishangilia baada ya kuingia fainali. |
Mashabiki wa Machester United wakiimba kwa furaha |
Warembbo wa Chelsea walikuwepo kuwakilisha |
Wachezaji wa timu za mashabiki wa Manchester United na Barcelona wakichuana vikali katika mchezo wao wa fainali ambapo Manchester United ilishinda mchezo huo. |
Mchuano mkali ukiendelea kwenye viwanja vya TCC Sigara. |
Mambo ya mnyama na burudani ileile |
Vinywaji vilikuwa vya kutosha kama vinavyoonekana katika picha |
Mashabiki wa timu ya Chelsea wakishangilia mara baada ya kuingia nusu fainali. |
Mashabiki wa Barcelona wakishangilia baada ya kuchukua ushindi wa pili katika bonanza hilo |
Saturday, July 14, 2012
HATIMAYE DAVID HAYE AMKATA KILIMI CHISORA AMTANDIKA KWA KNOCK OUT
Mwanasumbwi David Haye akimuadhibu
Chisora kwenye mpambano wao uliofanyika usiku wa kuamkia leo jijini
London kwenye uwanja wa Upton Park..
Mabondia wawili raia wa Uingereza
wamekuwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe tangu walipotwangana kwenye
mkutano wa waandishi wa habari jijini Munich wakati Chisora alipokuwa
akipigana na Klitschko, hivyo baada ya maneno maneno leo wakapnda
ulingoni na kumaliza ubishi na mwisho wa siku Haye akaibuka mshindi kwa
kumtwanga kwa knock out kwenye raundi ya tano.
AMIR KHAN ADUNDWA NA DANNY GARCIA ALFAJIRI YA LEO
Baada ya kuanza vizuri mpambano hatimaye Khan akaanza kupokea kipigo kutoka kwa Garcia. |
Garcia akimtandika ngumi za kumwaga Amir kHAN |
No comments:
Post a Comment