Arsenal yamwangusha Alexis, Mourinho afurahia - Mwanzo mwisho dirisha la usajili
Meshack Brighton
Getty
Dirisha la usajili wa Majira ya joto lilikuwa la kuvunja rekodi kwa matumizi lakini nani alikuwa na furaha Uingereza na nani alipatwa na huzuni?
WASHINDI: MAN UTD NA MOURINHO
Romelu Lukaku Manchester United
Katika uhalisia duniani kote Jose Mourinho atakuwa amepata mshambulizi wa ziada kwenye safu yake ya ushambuliaji zaidi ya Marcus Rashford na Anthony Martial waliokuwepo tangu mwanzo. Gareth Bale na Ivan Perisic walihusishwa na tetesi za kutaka kutua Old Trafford lakini United iliamua kusajili wachezaji wengine. Klabu hiyo imeridhishwa na usajili wao katika soko la uhamisho.
Nemanja Matic alitua kwa kitita cha £40 milioni na si tu kwamba ameleta uwiano mzuri kwenye timu lakini pia amempa uhuru zaidi Paul Pogba kuleta ushawishi mkubwa kwenye mchezo.
Romelu Lukaku ameanza kampeni kwa kufunga mabao matatu mechi za mwanzo. Atakuwa miongoni mwa wachezaji vinara wa Ligi Kuu Uingereza ifikapo mwisho wa msimu na ataisadia zaidi safu ya mashambulizi ya Mourinho.
Victor Lindelof bado hajaanza kazi yake lakini hatapata tabu kuzoea soka la Uingereza. Ataimarisha beki ya kati ya United kwani atakuwa na ushirikiano mzuri na Eric Bailly.
Kwa ufupi ni msimu bora wa majira ya joto kwa United.
WASHINDI: WEST BROM
Krychowiak Poland
Grzegorz Krychowiak alisajiliwa PSG msimu uliopita majira ya joto na mambo hayakumwendea vizuri mchezaji huyo wa kimataifa wa Polandi katika Parc des Princes, lakini bado ni kiungo mwenye uwezo mkubwa. Ataisaidia West Brom na kumpa Tony Pulis utawala zaidi dimbani.
Kieran Gibbs ni mchezaji mwenye uzoefu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa alioupata kutoka Arsenal na amecheza katika kiwango cha hali ya juu katika kipindi cha miaka kumi. Ni mchezaji mwenye weledi na mbinu kama beki wa kushoto.
Oliver Burke alikuwa moja ya wachezaji muhimu katika soko la Ulaya msimu uliopita kabla ya kuamua kujiunga na RB Leipzig lakini alishindwa kuzoea mazingira ya Bundesliga. Bila shaka wakati huuu ataweza kufanya maajabu soka la Uingereza.
MSHINDI: PAUL CLEMENT
Paul Clement Swansea City
Usajili pekee wa mwaka na umewagharimu €8.5m lakini bado mashabiki wa Swansea City hawatajiona wanyonge baada ya kumsajli Renato Sanches kutoka Bayern Munich.
Sanches alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotwaa taji la Euro msimu uliopita wa majira ya joto akiwa na Ureno na alikuwa mchezaji bora kinda wa michuano hiyo. Na alikuwa kijana wa dhahabu "Golden Boy" lakini alishindwa kutakata Bayern.
Paul Clement: Meneja huyo wa Swansea ametumia muda mwingi katika soka pembeni mwa Carlo Ancelotti na amefanikiwa kumpata Sanches kwa upendeleo.
KILAZA: ANTONIO CONTE
Antonio Conte Chelsea
Antonio Conte aliondoka Juventus kwa fedheha waliposhindwa kumpatia wachezaji aliowataka kwenye soko la usajili 2014. Aliwapatia mataji matatu mfululizo lakini alihisi wasingeweza kupiga hatua kubwa bila ya kusajli wachezaji aliokuwa akiwataka. Haikuwezekana na aliamu kuondoka.
Chelsea walicheza kwa moto msimu uliopita lakini hawajafanikiwa kuimarisha tena kikosi chao kilichotwaa taji Ligi Kuu Uingereza. Alvaro Morata, Tiemoue Bakayoko na Antonio Rudiger walisajiliwa kuchukua nafasi ya Diego Costa, Nemanja Matic na John Terry. Wachezaji muhimu kuimarisha kikosi chake lakini Conte lakini bado hajaridhika.
Romelu Lukaku alikuwa kwenye malengo yake lakini Manchester United ilimpiku. Fernando Llorente aliamua kutua Spurs. Alex Oxlade-Chamberlain alitimkia Liverpool. Dakika za mwisho kabisa kabla ya kufungwa dirisha la usajli bado walikuwa kwenye mazungumzo na Riyad Mahrez na Ross Barkley lakini mchezaji huyo wa Everton aliamua kuitosa Chelsea.
Danny Drinkwates amewasili akitokea Leicester City, lakini £35m ni nyingi sana kwa mchezaji huyo.
Swala la Costa bado halijatatuliwa yote ni kwa sababu ya mawasiliano duni ya Conte mwishoni mwa msimu. Matic aliruhusiwa kuondoka kujiunga na mahasimu wao. Na bado Chelsea hawajapata mbadala.
VILAZA: EVERTON
Wayne Rooney Everton
Juu juu mashabiki wa Everton wana mengi ya kujivunia. Wamepata mmiliki mpya Farhad Moshiri, ambaye ameahidi kutumia fedha nyingi kufanya usajili na meneja hakuona sababu ya kutoimarisha kikosi chake. Wameleta wachezaji wazawa wenye uwezo wa hali ya juu Jordan Pickford na Michael keane na Steve Walsh mkurugenzi wa soka ambaye alifanya usajili uliotwaa taji Leicester.
Lakini kama ukienda ndani zaidi kidogo utabaini mambo si shwari sana. Usajili wa Pickford, Keane na Davy Klaassen unawawezesha kuziba nafasi ya Joel Robles, ambaye hajawahi kuwa katika ubora, John Stone ambaye nafasi haikuwa imepata mbadala msimu uliopita, na Gareth Barry.
Pamoja na mauzo ya Lukaku £90m kwenda Manchester United, bado kurejea kwa Wayne Rooney hakuna tija kwao. Lukaku alikuwa akiimarisha timu jambo ambalo Rooney hataweza ukizingatia anatimiza miaka 32 mwezi Oktoba.
Mrithi wa Romelu Lukaku, Sandro hana viwango vya kuwa mshambuliaji bora duniani na atalazimika kufanya juhudi nyingi kuifikia shughuli ya Mbelgiji huyo aliyeondoka.
KILAZA: ALEXIS SANCHEZ
No comments:
Post a Comment