Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Uingereza klabu ya Leicester City, leo May 7 2016 baada ya mchezo dhidi ya Everton katika uwanja wao wa King Power walipokea Kombe lao la kwanza la Ligi Kuu Uingereza baada ya wiki iliyopita Tottenham Hotspurs kutoa sare ya 2-2 na Chelsea, hivyo Leicester ikatwaa taji hilo moja kwa moja.
Hili ndio Kombe la kwanza la Ligi Kuu kwa klabu ya Leicester City iliyoanzishwa miaka 132 iliyopita, lakini hili ndio taji la kwanza la Ligi Kuu kwa kocha wao Claudio Ranieri ambaye amewahi kuvifundisha vilabu ya Napoli, Inter Milan, Chelsea, Atletico Madrid na Juventus bila kuvipa taji la Ligi Kuu.
Leicester City wamekabidhiwa taji lao baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Everton, uliyomalizika kwa Leicester City kuibuka na ushindi wa goli 3-1, magoli ya Leicester City yalifungwa na Jamie Vardy dakika ya 5 na 65 kwa mkwaju wa penati na Andy King dakika ya 33, goli pekee la Everton lilifungwa na Kevin Mirallas dakika ya 88.
No comments:
Post a Comment