http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Sunday, December 20, 2015

NDEGE YA UFARANSA YATUA GHAFLA MOMBASA KWA KUHOFIWA KUWA NA BOMU


151220072609_air_france_624x351_reuters_nocredit
Ndege ya Air France ikiwa imetua
Mombasa, Kenya
Ndege kubwa ya abiria, Boeing 777 AF463, mali ya Shirika la Ndege la Ufaransa (Air France) iliyokuwa ikitokea Visiwa vya Mauritius kuelekea Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle, Paris, Ufaransa, imelazimika kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Mombasa baada ya kuhofiwa kuwa ndani yake kulikuwa na bomu.
Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, Jenerali Joseph Boinnet kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, imeeleza kuwa ndani ya ndege hiyo kulikuwa na abiria 473 na wahudumu 14 ambapo ndege hiyo ilitua salama na abiria wote kuokolewa.

5983902-Photo-399800Mwonekano wa ndege hiyo
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, mhudumu mmoja wa ndege hiyo aligundua kitu kinachofanana na bomu ndani ya choo cha ndege na kumtaarifu rubani aliyelazimika kuomba kutua kwa dharura kwenye uwanja huo, majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo (Jumapili).FranceeMwonekano wa Uwanja wa Ndege wa Mombasa.
Baada ya abiria wote kuokolewa, kitu hicho kinachodhaniwa kuwa ni bomu, kilitolewa na maafisa wa polisi kisha shughuli za kawaida zikaendelea uwanjani hapo wakati polisi nao wakiendelea na uchunguzi wao. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa abiria wawili wanashikiliwa na polisi kufuatia tukio hilo.
Chanzo BBC, mashirika ya habari.

No comments:

Post a Comment