Wakati
mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Yanga kesho wanacheza mechi yao ya
kwanza dhidi ya timu daraja la kwanza ya Ankara Seker Spor, uongozi wa
timu hiyo leo utatangaza jina la kocha mkuu katika mkutano na waandishi
wa habari.
Mechi
hiyo itachezwa saa 9.00 za Tanzania kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Mashindano wa kimataifa wa Yanga, Seif “Magari” Ahmed amesema kuwa
mazoezi ya jana yalifanyika asubuhi kutokana na jua kuwahi kuzama na
hali ya hewa kubadilika.
Ahmed
alisema kuwa wachezaji wanaendelea vizuri na mpaka sasa wamepania
kufanya vyema katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa
kusisimua.
Alisema
kuwa baada ya mechi hiyo, timu hiyo itaendelea na mazoezi kabla ya
kucheza mechi nyingine mbili na timu za madaraja ya juu.
“Timu
imeanza kambi rasmi, na mazoezi mazuri na maandalizi yametupa moyo japo
ka siku ya kwanza, kesho (leo) watacheza mechi ya kirafiki ya kwanza na
timu ya daraja la kwanza, n mechi nzuri kwani timu hiyo inashika nafasi
za juu katika ligi hiyo,” alisema Seif.
Alisema
kuwa kwa sasa timu yao inakaa mji mwingine tofauti na Antalya ambao upo
kilometa 70 kutoka mji wao wa zamani. Wamefikia hotel ya ufukweni
ijulikanayo wa jina la Suino Beach Hotel and Site ambayo ina hadhi ya
kimataifa.
Wakati
huo huo; uongozi wa klabu hiyo kesho utamtambulisha kocha mkuu wa
klabu hiyo katika mkutano maalum na waandishi wa habari makao makuu ya
klabu hiyo.
Seif alisema kuwa wamepitisha majina matano na walikuwa kwenye makubaliano nao mmoja wao ambaye kesho (leo) tutamtangaza rasmi.
Alisema kuwa wamepata kocha mzuri ambaye anajua mazingira ya Afrika na anajua maisha ya mpira kwa bara hili.
No comments:
Post a Comment