Vilio na majonzi vimetawala katika eneo la ajali
wakati wananchi wakijaribu kuwatambua ndugu na jamaa zao waliofariki
baada ya miili yao ikiwa imepangwa chini katika tukio hilo huku juhudi
nyingine za wananchi wakishirikiana na jeshi la polisi wakijaribu kutoa
mabaki ya gari katikati ya barabara ambapo kamanda polisi mkoa wa
morogoro faustine shilogile akizungumza katika eneo la tukio amesema
chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa noah alikua
kaijaribu kupita gari jingine bila tahadahari na kusababisha ajali ya
uso kwa uso.
Baadhi ya mashuhuda waliofika katika tuki hilo
akiwemo mkuu wa wilaya ya mvomero antony mtaka na mwenyekiti wa kijiji
cha ranchi ya wami dakawa wamelalamikia matukio mengi ya ajali za
mara kwa mara katika barabara hiyo na hivyo kuwakumbusha madereva
kuchukua tahadhari na kuomba mamlaka husika kuona umuhimu wa kuweka
alama za tahadhari pamoja na matuta katika eneo hilo.
Nae daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali ya
mkoa wa morogoro dr. Fransis samwene amethibitisha kupokea majeruhi wa
ajali hiyo na wawili bado hali zao ni mbaya.
No comments:
Post a Comment