Kwenye
Uwanja wa Chamazi Complex, Azam na Mbeya zilikuwa zikicheza huku uwanja mzima
ukiwa umejaa mashabiki wa Mbeya City, Yanga na Azam wenyewe hali iliyonogesha
pambano hilo lililokuwa kali na la aina yake.
Azam
ilikuwa ya kwanza kupata baoa dakika ya 13 mfungaji akiwa Humphrey Mieno aliyefunga
kwa kichwa akiunganisha mpira wa faulo ulipoigwa na Farid Mussa. Mbeya City
ilisawazisha bao hilo dakika ya 30 kupitia kwa Mwagane Yeya ‘Teacher’
aliyeunganisha vyema krosi ya Deus Kaseke.
Mabao
hayo yalidumu hadi mapumziko na katika kipindi cha pili, Mbeya City walipata
bao la pili dakika ya 52 mfungaji akiwa Yeya akimalizia kazi nzuri ya Steven
Mazanda. Bao hilo lilidumu kwa dakika nane tu kwani dakika ya 50, John Bocco aliisawazishia Azam akimalizia krosi ya Kipre
Tchetche.
Mbeya
City ilipata bao la tatu dakika ya 72 MFUNGAJI AKIWA Yeya tena kabla ya Khamis
Mcha kuisawazishia Azam dakika ya 83 na kufanya matokeo kuwa mabao 3-3.
Wachezaji wa Mbeya City wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mchezo
Mashabiki
wakiwa katika misururu mirefu kuingia uwanjani kushuhudia pambano la
Azam na Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Golikipa
wa Mbeya City, David Buruan akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa
langoni mwake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya
Azam FC unaoendelea kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Mbeya City.
No comments:
Post a Comment