Sunday, October 20, 2013
Uwepo wa al-Shabaab Mtwara unaibua tahadhari ya usalama nchini Tanzania
Kukamatwa kwa washukiwa 11 wa al-Shabaab waliokuwa wakifanya mafunzo ya kijeshi katika mkoa wa Mtwara mapema mwezi huu kumeibua wasiwasi miongoni mwa wachambuzi wa usalama na maofisa kwamba kikundi hicho cha wanamgambo kinajaribu kudanganya walalamikaji wa Tanzania katika jitihada za kupanua eneo lake la ushawishi.
Washukiwa hao walikamatwa katika mlima wa Makolionga katika wilaya ya Nanyumbu tarehe 7 Oktoba na walikutwa wanamiliki silaha za moto, mapanga na DVD 25 zenye miongozo ya mafunzo ya al-Shabaab, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara Zelothe Stephen.
"Moja ya DVD waliyokutwa nayo ilikuwa na programu yenye jina Zinduka Zanzibar," aliiambia Sabahi, maana yake "Amka Zanzibar". "Ilifundisha namna ya kuua kwa haraka na kutoa mafunzo kwa wanamgambo. DVD nyingine zilikuwa na mafunzo yanayohusu ugaidi yanayohusiana na al-Shabaab."
Mamlaka za ndani zinachambua ushahidi huo na kuwatafuta washukiwa wengine katika eneo hilo pamoja na msaada wa vyombo vya upelelezi kutoka makao makuu ya polisi huko Dar es Salaam, Stephen alisema.
Jina lake ni Mohammed Makande mwenye umri wa miaka 39 kama kiongozi kinara wa washukiwa waliokamatwa. Washukiwa wengine walibainishwa kama: Said Mawazo (miaka 20), Ismail Chande (miaka 18), Abdallah Hamisi (miaka 32), Ramadhani Rajabu (miaka 26), Salum Wadi (miaka 38), Hassan Omary (miaka 39), Fadhili Rajabu (miaka 20), Abbas Muhidini (miaka 32), Issa Abeid (miaka 21) na Rashid Ismail (miaka 27).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment