|  | 
| 
Familia ya mchezaji 
Mesut Ozil imetishia kumshataki raisi wa  Real Madrid  Florentino Perez 
juu ya madai kwamba mahusiano yake na mrembo wa kivenezuela yalimfanya 
ashuke kiwango alipokuwa Santiago Bernabeu.  
Baba yake Ozil, Mustafa 
alimshambulia vikali Perez, huku mwanae akiwa anatambulishwa rasmi 
kwenye klabu yake ya Arsenal na kuanza mazoezi, Mr. Mustafa Ozil alisema
 kwamba hatua za kuanza kumshtaki zimeanza.  
Mzee huyo ameonekana 
kukasirishwa vibaya kufuatia taarifa zilizochapishwa na gazeti la 
kihispania Marca kwamba Perez amesema kiwango cha Ozil akiwa na Real 
Madrid kilishuka kufuatia kuhangaika kwake na mpenzi wake ambaye ni 
mrembo wa zamani wa Venezuela, Aida Yespica. 
Ozil Snr pia 
alikasirishwa na mawazo kwamba ubinafsi wake wa kutaka fedha nyingi 
zaidi ndio uliochangia mjerumani huyo kujiunga na klabu ya Arsenal 
akitokea Madrid.  
‘Ni wazi Perez sio 
mwanadamu mwenye heshima, anaweza kuwa na fedha nyingi lakini hilo 
halimfanyi kuwa mtu mwenye heshima na adabu.  
'Anajaribu kufanya 
kwamba Mesut hakuwa mweledi kutoka na staili ya maisha yake akiwa Madrid
 na mimi baba yake nina uroho wa fedha tu. Haya yote ni ya uongo, na 
ndio maana nafikiria kumshtaki.  
‘Tutaangalia kila kitu, 
mawakili wameanza kuangalia kama kesi itakuwa na nguvu au la kabla ya 
kuangalia mbele, na baada ya hapo tutaamua hatua za kisheria za 
kuchukua.  
‘Anataka kumgeuza Mesut 
mbuzi wa kafara na kuonyesha kwamba ana mzazi mroho wa fedha, wakati hay
 mambo yapo mbali na ukweli. Tupo tayari kujitetea, kwa sababu 
ninachokitaka kwa mwanangu ni kufanikiwa. Hilo ndilo limekuwa jukumu 
langu siku zote.’ | 
Thursday, September 12, 2013
MESUT OZIL AANZA RASMI MAZOEZI ARSENAL HUKU FAMILIA YAKE IKITISHIA KUISHTAKI REAL MADRID
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
 





 
No comments:
Post a Comment