Askari
Polisi wakimzuia Kiungo Mkabaji wa Yanga, ambaye ni majeruhi, Athuman
Idd 'Chuji' aliyechukizwa na uchezeshaji mbovu wa mwamuzi wa mchezo kati
ya Yanga na Coastal, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam, leo jioni.
Chuji
alikuwa akimsaka mwamuzi huyo ili kumtia adabu kutokana na maamuzi yake
ya kuwapa penati wapinzani wao ambayo wao waliielezea kuwa haikuwa
sahihi. Mwamuzi huyo Martin Saanya, alitoa penati katika dakika ya 90+
kwa kile kilichoonekana kuwa Beki wa Yanga David Luhende aliunawa mpira
huo, huku mshika kibendera wake akiwa karibu kabisa na eneo la tukio na
kushindwa kutoa maamuzi kwa kumsaidia mwamuzi wake ambaye alipuliza
kipyenga cha kuashiria mkwaju wa penati hiyo iliyowakasilisha mashabiki
na wachezaji wa Yanga.
Katika
mchezo huo Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia
mshambuliaji wake, Didier Kavumbagu, katika dakika ya 68, kufuatia pasi
nzuri iliyopigwa na David Luhende, na Coastal, walisawazisha bao hilo
kwa mkwaju huo wa penati uliopigwa na Jerry Santo.
HUKO KWINGINEKO Matokeo ya mechi za leo ni:-
Rhyno 0-Azam 2, Oljoro 0- Simba 1, Tanzania Prisons 0- JKT 3, Ruvu
Shooting 1- Mbeya City 2, Mgambo Shooting 1- Ashanti Utd 0, Mtibwa Sugar
1- Kagera Sugar 0
Kipa wa Coastal Union, Shaban Kado, akiruka kuokoa moja ya hatari langoni kwake.
Beki
wa Coastal, Juma Nyoso (wa pili kushoto) akiondosha hatari, huku
wachezaji wa Yanga, Hussein Javu (kushoto) na hamis Thabit, wakiwania
mpira huo.
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (katikati) akiwatoka mabeki wa Coastal.
Mabeki wawili wa Coastal, wakimdhibiti David Luhende.
Didier
Kavumbagu, akishangilia bao lake sambamba na Simon Msuva. Katika mchezo
huo mwamuzi alitoa kadi nyekundu kwa wachezaji wawili Simon Msuva na wa
Coastal.
Askari
Polisi wakilinda mlango wa Chumba alichoingia Mwamuzi wa mchezo huo
baada ya kuona usalama wake matatani, ambapo Chuji alijaribu kupangua
ngome hiyo ili kuufikia mlango huo bila mafanikio.
No comments:
Post a Comment