Minong'ono ilikithiri kwa miaka
mingi. Wengi wakasema sio mjanja . Anapenda kucheza Golf sana . Ndio ni
jasiri kwa uhakika , lakini mtu asiye na mikakati.
Huyu ndiye mwanasiasa aliyejaribu mara tatu kuwa rais wa Zimbabwe lakini hakuwahi kufua dafu hata siuku moja.Hata ikiwa madai anayoyatoa kuwa kura ziliibwa na chama tawala ZANU-PF yatathibitishwa na majirani wa Zimbabwe wakitaka uchaguzi kurejelewa, rais Robert Mugabe hajaona sababu kubwa ya kuhofia upinzani mkubwa kwa utawala wake.
Sasa kwa nini Tsvangirai alaumiwe?
Wadadisi wanasema kosa kubwa ambalo yeye na chama cha MDC walifanya, ni uamuzi wake wa kujiondoa kutoka kinyang'anyiro cha mwaka 2008 kwa sababu ya ghasia zilizotokea baada ya utata uliofuata uchaguzi huo na kujiunga na rais Mugabe katika serikali ya Muungano.Na kama wanavyosema , Tsvangirai alimuwezesha mpinzani wake kushikilia wadhifa wakati yeye mwenyewe hakuwa na ushawishi mkubwa.
Hatua ya Tsvangirai ilizua utata mkubwa na kupingwa na washirika wake wa karibu wa MDC - ingawa kunao wanaosema kuwa hatua yake ilikuwa sawa.
Kwa kujiunga na serikali ya Muungano, Tsvangirai alionekana kutojali maslahi ya wafuasi wake wakati yake akiyapa kipaombele.
Hata hivyo kosa kubwa ambalo Tsvangirai alifanya ni kutojitetea wakati akiwa katika serikali ya Muungano na Mugabe.
Uhusiano wa dhuluma
Katika siku ya kwanza ambapo makamanda wa jeshi la Mugabe walipokataa kumpigia saluti kama waziri mkuu wa Zimbabwe, Tsvangirai angeteta na kupinga hilo na kisha kuwaambia wanadiplomasia waliokuja kwenye mkutano huo, walikuwa wanapoteza muda na kisha kujiondoa kwenye mkataba wa kugawana mamlaka.Lakini kwa kukosa kujiondoa, alimuonyesha Mugabe kuwa angeendelea kuwa katika serikali ambayo haimpi heshima zake na yeye ni mwanachama mwenye ushawishi mdogo katika serikali ya Muungano na kuwa angestahimili dhuluma katika uhusiano wao ambao ulifika mwisho wake wiki jana.
Bwana Tsvangirai badala yake aliendelea kusisitiza umuhimu wa kupatanisha watu akiwa na matumaini kuwa Mugabe angezingatia demokrasia.
Baadhi wanasema kuwa Tsvangirai angejiondoa kwenye uchaguzi kabla ya uchaguzi kufanyika wakati ilipokuwa wazi kuwa Mugabe hangetoa muda kwa wapiga kura kujiandaa kwa uchaguzi, mfano kujisajili au hata kufichua daftari la wapiga kura ambalo wengi wanasema lilikuwa na dosari nyingi.
Lakini badala yake Tsvangirai aliitikia wito wa Mugabe wa kufanyika uchaguzi ambao sasa anasema ulijaa makosa na wizi wa kura.
Je ilikuwa hatua nzuri au ilikuwa ishara ya kutojua au kujiamini kupita kiasi?
Wakati mmoja hilo swali litajibiwa na wakereketwa wa chama chake na mwishowe wapiga kura.
No comments:
Post a Comment