KOCHA Arsene Wenger yuko tayari kubomoa benki ya Arsenal kwa ajili ya kuvunja rekodi ya usajili wiki hii kwa kununua nyota watatu wa Ulaya.
Habari
kwamba inafikiria kwa mapana kuwasajili nyota wa Real Madrid, Gonzalo
Higuain, wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan na wa Bayer Leverkusen,
Lars Bender, zitakuwa faraja kubwa kwa mashabiki wa Arsenal baada ya
miaka ya huzuni kwa kukosa mataji.
Uhamisho mkubwa: Arsenal inamtaka mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis aliahidi kutoa fedha za kutosha
wiki iliyopita kwa ajili ya usajili na Wenger anaamini anaweza kupanua
timu yake hadi kuwa na uwezo wa kushindania mataji.
Kocha
huyo wa Arsenal anaamini kustaafu kwa Sir Alex Ferguson katika klabu ya
Manchester United ni nafasi nzuri kwa klabu yake kurejea kwenye anga za
mataji na anatarajia usajili wa Muargentina Higuain utakuwa wa gharama
zaidi, Pauni Milioni 25.
Wenger
anataka kuimarisha safu yake ya kiungo kwa kumsajili chaguo lake la
kwanza Gundogan wa Borussia Dortmund aliyefunga bao la kusawazisha kwa
penalti katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich iliyoshinda 2-1 Uwanja wa Wembley, ambaye atamgharimu Pauni Milioni £20.
Lakini
pia anaweza kuhamia kwa nyota wa Bayer Leverkusen anayeuzwa Pauni
Milioni 17, Bender iwapo atamkosa Gundogan. Yeyote atakayesajiliwa kati
ya hao, atavunja rekodi ya dau kubwa la usajili la Arsenal la Pauni
milioni 15, zilizotumika kwa uhamisho wa Andrey Arshavin mwaka 2009.
Chaguo la kwanza la Wenger: Ilkay Gundogan wa Borussia Dortmund
Arsenal pia italazimika kusaka sentahafu mwingine baada ya kuwa tayari kumpiga bei Nahodha wake, Thomas Vermaelen.
No comments:
Post a Comment