MWANASOKA bora wa zamani wa dunia,
Zinedine Zidane amesema Real Madrid watavunja rekodi ya dunia ya usajili
kwa kumsaini Gareth Bale.
Winga huyo wa Tottenham amekuwa
akihusishwa kwa kiasi kikubwa kuhamia kwa wababe hao wa Hispania katika
Jiji la Madrid walio tayari kutoa Pauni Milioni 85.
Hiyo itavunja rekdi ya usajili ghali kwa
mchezaji ya Pauni Milioni zilizotumika kumsaini aliyekuwa mchezaji wa
Manchester United, Cristiano Ronaldo miaka minne iliyopita.
Anatakiwa: Winga wa Tottenham, Gareth Bale yupo kwenye rada za Real Madrid kwa Pauni Milioni 85
"Mazungumzo kuhusu Gareth Bale si ya
kushitukiza," amesema Zidane, ambaye ni Mkurugenzi wa Michezo Madrid na
kuongeza watapanda dau zaidi iwapo itatokea klabu ya kutaka kushindana
nao kuwanai saini ya mchezaji huyo.
"Kuna klabu nne au tano kwa sasa ambazo
zina uwezo wa kifedha kumsajili, lakini si kwa kuvunja rekodi ya ada ya
uhamisho kama hivyo,"aliongeza.
Mtu wa mipango: Zinedine Zidane (katikati) amesema atapambana kumsaini Bale majira haya ya joto
Dau hilo kubwa haitakuwa rahisi kwa
Spurs kukataa kumuuza na bosi wa Bernabeu, Florentino Perez amemlenga
nyota huyo wa Wales kama chauo lake kuu.
Bale anaweza kuchukuliwa Madrid akazibe nafasi ya Ronaldo ambaye amekuwa akihusishwa na kurejea Old Trafford.
Wakati huo huo, Viongozi wa Juventus
wamefanya mazungumzo na Madrid kuhusu Gonzalo Higuain jana. Wataliano
hao wanataka kuipiku Arsenal kumsaini Muargentina huyo anayeuzwa Pauni
Milioni 20, lakini wameambiwa dili hilo itabidi lisubiri hadi Carlo
Ancelotti apewe mikoba ya ukocha.
No comments:
Post a Comment