KLABU
ya Chelsea imehamishia mawindo yake kwa mshambuliaji wa Borussia
Dortmund, Robert Lewandowski katika harakati za kocha Jose Mourinho
kusaka kiongozi wa safu ya ushambuliaji.
Mourinho
hashawishiki na Fernando Torres na Demba Ba na wanataka mtu mwingine
katika safu ya ushambuliaji kupambana na nyota kinda, Romelu Lukaku na
mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 18, Andre Schurrle ambaye
wazi atakuwa anacheza pembeni.
Lewandowski
anataka kuachana na wana fainali hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu
huu, lakini Dortmund imegoma kumuuza kwa wababe wao, Bayern Munich,
ambako alichagua.
Atatua England? Lewandowski anatarajiwa kuhama baada ya kufanya vizuri kwa misimu kadhaa Ujerumani
Hashawishiki: Mourinho haoni kama washambuliaji wake watatosha kuiweka timu kileleni
Mwakilishi
wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amewasiliana na Chelsea,
Manchester United, Real Madrid na Barcelona pamoja na Bayern juu ya
uhamisho wa Pauni Milioni 25.
Dortmund
haiko tayari kumuuza kwa Bayern, baada ya mabingwa hao wa Ujerumani na
Ulaya kuwachukulia mchezaji wao mwingine, Mario Gotze kwa dau la Pauni
Milioni 32 mwezi uliopita.
Wiki iliyopita, Mtendaji Mkuu wa klabu, Hans-Joachim Watzke aliliambia Bild: "Robert Lewandowski hatauzwa kwa FC Bayern mwaka 2013. Hiyo ni mwisho. Tumemuambia Robert na wakala wake sasa,"alisema.
Suluhisho la ushambuliaji: Lewandowski anaweza kuwa suluhisho jepesi kwa Cavani (kushoto) wakati Schurrle atacheza pembeni.
Hiyo
inaweza kufungua milango kwa Chelsea, ambao wanaendelea taratibu
kuisaka saini ya thamani ya Pauni Milioni 54 ya mshambuliaji wa Napoli,
Edinson Cavani.
Cavani
anatakiwa kwa muda mrefu Chelsea, lakini Mourinho ni shabiki mkubwa wa
Lewandowski aliyemshuhudia akifunga mabao manne dhidi ya timu yake ya
zamani, Real katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Chelsea
bado pia inamfukuzia mshambuliaji wa Zenit St Petersburg, Hulk, lakini
Manchester United haiko tayari kumruhusu Wayne Rooney ahamie Stamford
Bridge.
No comments:
Post a Comment