KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Kesi Dikoroma na dada mmoja (jina halikupatikana mara moja) wamejikuta wakitapeliwa simu zao baada ya kupewa tenda ya kuchimba kaburi.
Wawili hao wamekutwa na mkasa huo hivi karibuni katika makaburi ya Ulongoni, Tabata-Segerea, jijini Dar, ambapo imeelezwa kuwa, Kesi ambaye hufanya shughuli za kuchimba makaburi, alipatwa na msala huo baada ya baba mmoja ambaye hakufahamika jina lake kufika makaburini hapo na kuwapa tenda feki ya kuchimba kaburi.
“Aliwaambia kuwa ana shida ya kuchimbiwa kaburi litakalogharimu shilingi laki tano na kudai anataka baada ya kuchimbwa lijengwe kabisa.
“Ndipo Kesi na huyo dada ambaye alipewa tenda ya kuchota maji, waliingia mzigoni huku mwingine akaambiwa akalete matofali na marumaru.
“Baada ya kuwapa tenda, bosi huyo alitegea yule dada alipokwenda kuchota maji na yule wa matofali alipoondoka, akakwapua simu ya yule kaka aliyekuwa chini akichimba kaburi na ya yule dada walizokuwa wameziweka pembeni ya kaburi akatoweka nazo,” kilisema chanzo makini.
Ilipofika jioni, mmiliki wa eneo lile aliamua kuzika mgomba kwani aliogopa kaburi kukaa wazi. Hata hivyo, wakazi wa eneo hilo wanadai kuwa waliporudi siku ya tano walikuta kwenye lile kaburi alishazikwa mtu mwingine.
No comments:
Post a Comment