


Usiku
wa kuamkia leo ujumbe ulisambazwa kwenye mitandao ya simu za mkononi na
mitandao ya kijamii, Facebook na Twitter kuwa Bi Kidude amefariki
dunia! Moja ya SMS hiyo ilisomeka: Qaallu Inna Lillahi Wainna Ilaihi
Raajiuni; BI KIDUDE AMEFARIKI DUNIA! Habari ambazo zimekanushwa vikali
na mwenyewe leo asubuhi. Kudhidirisha kweli hajafa, Bi. Kidude aliongea
moja kwa moja na Radio One na kumwambia mtangazaji aliyetaka kujua
ukweli wa habari hizo kwa kumjibu: "Maiti haiongei, mimi ndiye Bi
Kidude, mzimaaa!" HII NI TABIA AMBAYO INAKUWA KWA KAZI YA KUZUSHIA WATU
VIFO KWA KUTUMIA MITANDAO YA SIMU NA KIJAMII

No comments:
Post a Comment