Baada ya kuwasili London mapema jana,
timu zote hizo zilipata fursa ya kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa timu
ya taifa ya England, ambao utahimili vishindo vya fainali ya Ulaya kwa
mara ya pili ndani ya miaka mitatu.
Dortmund imerejea katika fainali ya Ligi
ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1997 walipoifunga Juventus
ya Italia mabao 3-1 kwa msaada wa kocha wa Aston Villa, Paul Lambert,
wakati Bayern inatumai kutwaa taji la tano la michuano hiyo baada ya
kufungwa na Chelsea kwenye fainali mwaka jana.
Ugeni: Kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp
(kushoto) akiwa Wembley na kocha wa Aston Villa, Paul Lambert, ambaye
aliiwezesha klabu hiyo ya Ujerumani kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa
mwaka 1997
Mjadala mzito: Bastian Schweinsteiger, Arjen Robben na Franck Ribery wakiwa Wembley
Wachezaji wa Bayern Munich wakiingia Wembley kufanya mazoezi jana
Nyota: Robben (kushoto) na Ribery kati ya majina makubwa Wembley jioni ya leo
Anarekebishwa: Mshambuliaji tegemeo wa Dortmund, Robert Lewandowski akirekebishiwa viatu vyake
Kiatu cha mabao: Kiatu cha Lewandowski fainali
Utatu mtakatifu: Kevin Groskreutz, Robert Lewandowski na Marco Reus wakiwa mazoezini Wembley jana
No comments:
Post a Comment