http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Wednesday, April 24, 2013

wanafunzi waandamana kutokana na kifo cha mwenzao na kupelekea chuo kufungwa mpaka board ya chuo itakapowarudisha









Jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia kimelazika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi waliodaiwa kufanya vurugu kufuatia tukio la kifo cha mwanafunzi mwenzao Henry Kago anayedaiwa kuuwawa na watu wasiojulikana jumanne hii majira ya saa 4 usiku katika eneo la CDA njiro Arusha
Hali hiyo imepelekea uongozi wa chuo hicho kutangaza kukifunga chuo kwa muda usiojulikana

Kuanzia majira ya saa 4 za asubuhi eneo la Njiro kilipo chuo cha uhasibu Ausha sauti za mirindimo ya mabomu ya machozi ndiyo iliyokuwa ikisiskika

Chanzo kinaelezwa kuwa ni tukio la kuuwawa kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili Henry Kago anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22 huku mazingira ya kifo chake yakiwa bado yamegubikwa na utata wanafunzi

Taarifa zinaeleza kuwa vurumai hizo zilianza majira ya saa tatu asubuhi ambapo wanafunzi walikuwa wamejikusanya kwa lengo la kuandamana kuelekea ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Arusha lakini mamlaka zinaeleza kuwa lengo la wanafunzi hao lilikuwa ni kufanya vurugu 
Mkuu wa mkoa wa Arusha aliyeiongoza kamati yake ya ulinzi na usalama walipozuru eneo la chuo,hakukuonekana unafuu wowote zaidi kuibuka kwa zomeazomea huku mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiingia katika tuhuma za kushinikiza wanafunzi kufanya vurugu
Kufuatia vurugu hizo uongozi wa chuo cha uhasibu Arusha kuputia kwa Naibu mkuu wa chuo taaluma Bw.Faraji Kasudi umetangaza kukifunga chuo kwa muda usiojulikana.

Mbunge Wa Arusha Mjini Godbless Lema Akiwatuliza Wanafunzi Wa Chuo Hicho
Vurugu  kubwa  zimeibuka  chuo  cha  uhasibu cha Arusha   baada ya mwanachuo kuchomwa kisu na mwanaakijiji na kufariki dunia....

No comments:

Post a Comment