Usaliti
ni kitu kibaya sana. Ni matokeo ya ukosefu wa ubinadamu. Ni kwenda nje
ya makubaliano ya kimsingi. Ni uamuzi wa mtu kushusha thamani yake
mwenyewe. Ni kujidhalilisha kwa makusudi. Ni kujionesha mbele ya umma
kwamba wewe hufai, huaminiki.
Aya
hiyo, ikupe mantiki kuwa msaliti siyo binadamu. Sasa basi, endapo
utaamua kufanya hivyo, ujijue kwamba unajidhalilisha na unajipa sifa
mbaya mbele ya jamii. Kwamba unajipeleka kwenye ukurasa ambao kila
atakayekusoma, atakutafsiri kuwa hufai, kwani huna maana.
Kwa nini
watu wanasaliti? Hapa nieleze kuwa usaliti ambao naujengea hoja siyo ule
wa kuchukua maneno upande mmoja na kupeleka sehemu nyingine, la hasha!
Namaanisha vitendo vya kumchepuka mwenzi wako. Yaani unakwenda kufanya
mapenzi nje ya ndoa au kuhusika na mtu tofauti na mchumba au mpenzi wako
anayekubalika.
Usaliti unasababishwa na vitu vingi lakini kikubwa ni
tamaa. Inawezekana ikasababishwa na hulka ya kutaka kuwa na wengi au
kuvutwa na fahari ya macho. Umemuona, akakuvutia kisha ukataka uone
ndani pakoje. Huu ni ulemavu mkubwa sana unaotawala vichwa vya wengi.
Fedha
ni janga kuu. Wanawake kwa wanaume wanaendeshwa na pesa, hivyo imekuwa
ikiamua hatma ya uhusiano wa watu wengi. Nilishawahi kuandika kuwa
“fedha ni dereva wa moyo”, kwamba mapenzi kwa sehemu kubwa yanaamuliwa
na fedha. Kama huna kitu, utasalitiwa tu!
Tuachane na kipengele cha
fedha na tamaa, kwa upande wa wanawake, zipo sababu mbalimbali ambazo
huwafanya wachepuke ama nje ya ndoa au ‘kuchutama’ kwa mwanaume wa
pembeni tofauti na boyfriend/mchumba wake. Sababu zao zipo kisaikolojia
zaidi.
Ni muhimu kwa kila mtu kutambua haya kwa sababu kuu mbili;
Mwanaume kujua namna ya kuishi vizuri na mwenzi wake ili ajue nyakati za
hatari za kusalitiwa. Pili, mwanamke kujichunga, kuvaa uimara wakati
wowote na kuepuka ushawishi wa kusaliti. Kuna ushauri muhimu sana ndani
ya makala haya.
Pamoja na sababu nitakazozieleza ambazo nyingine
zinaonesha kuwapendelea wanawake kwamba wakati mwingine husaliti
kutokana na tabia za wenzi wao, ila ukweli ubaki kwenye kipimo chake
kuwa msaliti yeyote anakuwa amejiondoa kwenye taswira halisi ya
ubinadamu na kujifananisha na mnayama.
Kitendo cha kuvua nguo mbele
ya mwanaume huyu, kesho eti kwa sababu umekosewa ndiyo ukafanya
hivyohivyo kwa mwingine, ni sawa na kujifananisha na wanyama. Pointi
hapa ni kuwa unajifananisha na wanyama kwa sababu wao huwa hawavai nguo.
Ni kama wewe tu unayevuavua ovyo na kuruhusu wanaume tofautitofauti
wakuone.
Wanyama huwa hawafanyi makubaliano ya kueleweka, isipokuwa
hupandana kiholelaholela. Nawe kwa sababu maisha yako hayapo kwenye
mtiririko unaokubalika, unaamua kufanya kama wanyama. Leo unatumika kwa
huyu, keshokutwa upo na mwingine. Inawezekana unafurahia maisha hayo
lakini siyo sawa kabisa. Hizo ulizonazo ni hulka za wanyama.
Kuhusu
sababu ambazo huwafanya wanawake kuamua kuziendea kinyume ndoa au
uhusiano wao wa kimapenzi na kufanya usaliti, soma sababu 10
zinazofuata. Ukisoma kinagaubaga, utaelewa wapi pa kushika na nini cha
kufanya. Ni mapenzi tu na mapito yake.
HISIA ZA KIPINDI CHA MPITO
Hiki
ni kipindi cha hatari sana kwa mwanamke. Kinaweza kutokana na sababu
mbalimbali ila muhimu kwa mwanaume wake ni kuwa makini sana.
No comments:
Post a Comment