Kikosi
cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na mazoezi asubuhi katika
uwanja wa mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa pili
wa Ligi ya Vodacom dhidi ya timu ya Polisi Morogoro siku ya jumamosi
Machi 30 ,2013 katika dimba la Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu
ya Vodacom kwa kuwa na pointi 48 na mabao 37 ya kufunga na mabao 12 ya
kufunga, iko mbele kwa pointi 11 zaidi ya timu ya Azam inayoshika nafasi
ya pili kwa kuwa na ponti 37 na mabao 32 ya kufunga na mabao 16 ya
kufungwa.
Mara baada ya kupata ushindi wa tano
mfululizo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom, kikosi cha mholanzi
Ernie Brandts kiliendelea na mazoezi katika uwanja wa mabatini
Kijitonyama siku ya leo ikiwa ni sehemu ya maandalzi ya mchezo wa siku
ya jumamosi.
Katika mchezo wa mwisho Young
Africans iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Ruvu Shooting
bao lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Hamis
Kiiza, tangu mzunguko wa pili uanze Yanga imeshacheza jumla ya michezo
saba na kufanikiwa kushinda michezo sita na kutoka sare mmoja hivyo
kujikusanyia pointi 19 kati ya 21.
Ili kujiweka
katika mazingira mazuri ya kutwaa Ubingwa, Kocha Mkuu Brandts amesema
anakianadaa kikosi chake kuhakikisha kinapata pointi 3 katika kila
mchezo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa Ubingwa.
"Kila
mchezo tunaocheza kwa sasa ni fainali kwetu, kila timu inahitaji kupata
pointi ili kujiweka katika nafasi nzuri, na sisi pia tunahitaji kupata
pointi 3 katika kila mchezo hali inayopelekea mechi kuwa ngumu, lakini
kikubwa nimekiandaa kikosi changu kuhakikisha kinaibuka na pointi 3
katika kila mchezo" alisema Brandts
Katika mazoezi
yaliyoanza tangu jana wachezaji wote wanaendelea kujifua, ambapo
wataendelea na mazoezi mpaka watakapoungana na wachezaji wenzao walioko
katika timu za Taifa mbalimbali.
Yanga imetoa
jumla ya wachezaji nane kwa ajili ya kuzitumikiia timu za taifa,
wachezaji hao ni Klevin Yondano, Frank Domayo, Saimon Msuva, Nadir
Haroub 'Cannavaro', na Athuman Idd 'Chuji'(Tanzania), Haruna Niyonzima,
Mbuyu Twite (Rwanda) na Hamis Kiiza (Uganda).
wachezaji wanaondelea na mazoezi ni :
Said Mohamed, Yusuph Abdul na Ally Mustafa 'Barthez' (magolikipa)
Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Salum Telela, Oscar Joshua, Godfrey Taita na Juma Abdul (walinzi)
Nurdin Bakari, Omega Seme na David Luhende, Reheni Kibingu (viungo)
Jerson Tegete, Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi
Ladislaus Mbogo, George Banda na Nizar Khalfani ni wagonjwa hawakuweza kufanya mazoezi leo
No comments:
Post a Comment