Na Edo Kumwembe
BAADHI ya mastaa wa kikosi cha kwanza, Simba (majina tunayo) wamesema hawana imani na mbinu za Kocha Mkuu Patrick Liewig na hilo limethibitika zaidi katika mchezo wao wa Angola.
BAADHI ya mastaa wa kikosi cha kwanza, Simba (majina tunayo) wamesema hawana imani na mbinu za Kocha Mkuu Patrick Liewig na hilo limethibitika zaidi katika mchezo wao wa Angola.
Mwishoni mwa wiki, Simba ilishambuliwa na kipigo 
cha mabao 4-0 kutoka  Recreativo Libolo ya Angola katika mchezo wa 
marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kuaga mashindano 
raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 5-1, kutokana na kufungwa bao 1-0 
katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita, Dar es Salaam.
Wakizungumza juzi usiku kwenye hoteli ya Ritz 
iliyopo mji wa Calulu lilikofanyika pambano hilo la marudiano, mastaa 
hao wamesema mfumo wa sasa wa Simba ni kujihami zaidi kuliko 
kushambulia.
"Mbinu nyingi tunazotumia ni za kujihami. 
Mazoezini hatufundishwi kucheza soka la kushambulia na badala yake kocha
 amekuwa akitumia muda mwingi kutufundisha namna ya kukaba maadui katika
 maeneo yetu."alisema mchezaji mmoja nyota katika nafasi ya kiungo.
"Mimi siyo msemeji, lakini sasa hivi inabidi 
niseme. Wachezaji vilevile hatuko fiti. Tunafanya mazoezi kwa dakika 
chache, hatujawahi kucheza mazoezi ya mechi miongoni mwetu. Uimara wa 
timu unaanzia mazoezini na sisi hatuko imara." aliongeza staa huyo.
Nyota mwingine wa Simba anayecheza nafasi ya 
ushambuliaji alisema: "Kutokuwapo Emmanuel Okwi na Patrick Mafisango 
(marehemu), siyo sababu ya timu kufanya vibaya. Nadhani kocha (Liewig) 
abadili mbinu."
"Kuna mechi nyingi Okwi hakucheza na bado 
tulishinda. Mimi sifurahishwi na jinsi tunavyocheza kwa kumtegemea 
mshambuliaji mmoja mbele." alisema mshambuliaji huyo.
Nyota mwingine wa safu ya ulinzi alihoji mantiki 
ya viongozi na Benchi la Ufundi kumsajili kipa wakati wa dirisha dogo, 
huku timu ikiwa na upungufu wa wachezaji katika safu ya ushambuliaji.
Aidha, kiongozi wa msafara wa Simba na Mjumbe wa 
Kamati ya Utendaji, Zacharia Hans Pope amekuja na hoja tofauti na 
malalamiko ya wachezaji dhidi ya kocha wao.
Hanspope amesema Simba imefungwa kwa sababu 
wapinzani wao Libolo walijiandaa vizuri kwa mazingira yote, ndani na nje
 ya uwanja kulinganisha na Simba.
"Yatasemwa mengi, lakini ukweli tumetolewa na timu
 yenye uwezo kuliko sisi. Wenzetu wamefanya maandalizi mazuri. Kumbuka 
kuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani waliwahi kuichapa Orlando Pirates ya 
Afrika Kusini 3-0." alisema Hans Pope.
 

 
No comments:
Post a Comment