Mlinzi wa kati wa timu ya Young Africans Ladislaus Mbogo anaendelea
vizuri baada ya jana kufanyiwa upasuaji wa uvimbe (shavuni) katika
Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam, upasuaji uliofanyika
chini ya usimamizi wa daktari wa timu ya Young Africans Dr Nassoro
Matuzya.
Mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi katika uwanja wa mabatini
Kijitonyama, wachezaji wote wa Young Africans pamoja na benchi la ufundi
waliongozana kwenda Hopsitali ya Mwananyamala kumpa pole Mbogo ambaye
jana alifanyiwa upasuaji wa uvimbe sehemu ya shavu la kushoto.
Akiongea leo asubuhi baada ya
kutembelewa na wachezaji na benchi la Ufundi, Mbogo amesema anajisikia
vizuri, anamshukuru mungu upasauji umeenda vizuri na hali yake
inaendelea kuimarika hivyo anaamini muda si mrefu atarudi katika hali
yake ya kawaida.
Mbogo ambaye alisajiliwa mwaka jana
katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012.2013 akitokea timu ya Toto
Africans, amekifikia hatua hiyo ya kukubali kufanyiwa upasuaji kufuatia
kufanyiwa uchuguzi na madakatari kutoka hospital ya Mwananyamala.
Dr Nassoro Matuzya akiongea kwa niaba ya madaktari waliomfanyia
upasauaji, amesema upasuaji ulifanikiwa kufanyika salama kabisa,
tulimfanyia upasuaji jana asubuhi kufikia mida ya mchana tayari tulikua
tumeshamaliza na kwa sasa yupo wodini kwa mapumziko chini ya uangalizi
wa madakatari.
Kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Dr Matuzya, Mbogo atakua nje ya uwanja
kwa kipindi kisichopungua wiki tatu akiendelea kuunguza sehemu
aliyofanyiwa upasuaji.
Katika hatua nyingine Kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi
yake katika uwanja wa mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo dhidi ya
timu ya Ruvu Shooting, mchezo utakaofanyika siku ya jumamosi katika
dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha wachezaji 25 kipo kambini katika hosteli za klabu zilizopo
mitaa ya Twiga/Jangwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo wa
jumamosi, mchezaji pekee ambaye hayupo kambini ni Ladislasu Mbogo ambaye
amedanyiwa upasuaji wa uvimbe sehemu ya shavu
No comments:
Post a Comment