| |
WATOTO wa Abedi Pele, Jordan na Andre, wametangaza wametangaza uamuzi wao wa kujiuzulu kwa muda kuchezea timu ya taifa ya Ghana. Wawili hao wametuma taarifa kwa Chama cha Soka Ghana FA jana.
Wote walikuwa wanadaiwa kuwa na mgogoro na viongozi wa FA.Andre Ayew
Andre Ayew ameelezea matatizo yake binafsi na uongozi ya timu ya Black Stars yamemfanya ajiuzulu kwa muda. Amesema amevunjika moyo na nguvu kutokana na matatizo yake na uongozi na kwamba hawezi kuitumikia Ghana vizuri kwa sasa.
"Uamuzi wangu wa kusitisha huduma zangu timu ya taifa unatokana na matatizo kadhaa yaliyojitokeza hivi karibuni, hususan juu ya uhusiano wangu na uongozi wa timu ya wakubwa ya taifa, Black Stars."
Jordan Ayew
Wakati huo huo, Ayew mdogo anafikiri hakubaliki. Amesema licha ya kufanya vizuri, inaonekana uongozi haumjali.
FA ya Ghana bado haijajibu barua za vijana hao, watoto wa gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment