http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Tuesday, February 26, 2013

NIYONZIMA AWAWEKEA NADHIRI KAGERA KESHO, ASEMA YANGA LAZIMA ILIPE KISASI CHA KAITABA


Haruna Niyonzma: Tutalipa kisasi kesho kwa Kagera
Na maulid
KIUNGO wa Yanga, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima, amesema kwamba watalipa kisasi cha kufungwa 1-0 na Kagera Sugar wakati watakaporudiana na timu hiyo kesho, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Niyonzima alisema kwamba wamepania kushinda mechi zote zilizobaki za Ligi Kuu ili kuchukua ubingwa kwa heshima kubwa.
Amesema kwanza lazima walipe kisasi cha kufungwa na Kagera katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu, mwaka jana Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
“Kagera walitufunga Bukoba, na sisi lazima tuwafunge hapa Jumatano. Lakini kikubwa ni kampeni yetu ya kushinda kila mechi ili tuchukue ubingwa kwa heshima kubwa,”alisema.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Rwanda, alisema wanaiheshimu Kagera Sugar ni timu nzuri na wanatarajia upinzani mkubwa, lakini kushinda lazima.
“Hakuna mechi nyepesi kwa hapa ligi ilipofikia na sisi tunalitambua hilo, hivyo Jumatano tunajua Kagera watakuwa wagumu sana, lakini tutawafunga tu,”alisema.  
Yanga inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 39, baada ya kucheza mechi 17, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 36 baada ya kucheza mechi 18, wakati Simba SC iko nafasi ya tatu kwa pointi zake 31, baada ya kucheza mechi 18 pia.
Niyonzima alikuwa shujaa wa Yanga katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu, dhidi ya wapinzani wao wakuu katika mbio za ubingwa, Azam FC baada ya kufunga bao pekee la ushindi.

MSIMAMO WA LIGI KUU BARA
                        P W D L GF GA GD Pts
1 Yanga 17 12 3 2 34 12 22 39
2 Azam 18 11 3 4 31 15 16 36
3 Simba SC 18 8 7 3 26 15 11 31
4 Coastal Union 18 8 6 4 21 16 5 30
5 Kagera Sugar 18 7 7 4 19 16 3 28
6 Mtibwa Sugar 18 7 6 5 21 18 3 27
7 Ruvu Shooting 16 7 4 5 20 17 3 25
8 Mgambo JKT 18 7 3 8 14 17 -3 24
9 JKT Oljoro 18 5 6 7 19 22 -3 21
10 Tanzania 18 4 7 7 11 16 -5 19
11 JKT Ruvu 17 4 4 9 14 27 -13 16
12 Toto African 18 2 8 8 14 25 -11 14
13 African Lyon 19 3 4 12 13 31 -18 13
14 Polisi Moro 17 2 6 9 8 18 -10 12

No comments:

Post a Comment