http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Thursday, February 28, 2013

MILOVAN AONDOKA BONGO - RAGE AKIMWAGIA LAWAMA KUHUSU USAJILI - CIRKOVIC AJIBU MAPIGO



ALIYEKUWA kocha wa Simba Milovan Cirkovic ameondoka nchini jana alfajili na shirika la ndege ya Uturuki baada ya kufanikiwa kulipwa fedha zake  alizokuwa anaidai klabu hiyo.

Kocha huyo ambaye alikuja nchini mapema mwezi huu kwa ajili ya kudai fedha zake baada ya kudanganywa na uongozi wa Simba kuwa wanamtamlipa fedha zake bila mafanikio yoyote ndipo aliamua kuja kudai mwenyewe.

Hata hivyo baada ya kusota muda mrefu huku viongozi wakiwa wanampa ahadi kila siku hatimaye jana alfajiri alifanikiwa kuondoka baada ya kulipwa deni lake  kutoka kwa Malkia wa nyuki Rahma Al Kharoos ambaye ni mjumbe wa kamati ya fedha na mfadhili wa klabu hiyo.

Kocha huyo ameondoka na rekodi ya ubingwa Simba ikiwa ni pamoja na rekodi kubwa ya ushindi ‘mnene’ wa mabao 5-0 dhidi ya watani wao Yanga, msimu uliopita.
 

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amesema kuwa uongozi wake haupaswi kulaumiwa kwa kusajili wachezaji wasio kuwa na uwezo bali anayetakiwa kulaumiwa ni aliyekuwa kocha wao Mserbia Milovan Cirkovic.

Rage alisema kuwa wachezaji wote waliowasajili msimu huu ni pendekezo la kocha huyo ambaye alitimuliwa raundi ya kwanza baada ya timu kutofanya vizuri katika michezo yake ya mwisho.

Alisema awali waliwaleta wachezaji wawili kutoka Cameroon lakini kocha aliwakataa na kuwasajili wachezaji wake ambao aliwataka yeye.

Aliongeza kuwa haoni sababu ya wao kulaumiwa kwa sababu wao ni uongozi na sio wachezaji na kuongeza kuwa kama watu wanawalaumu wao wanacheza namba ngapi uwanjani.

Rage akiwa anatoa kauli hiyo tayari kocha Milovan kwa upande wake alikwisha sema kuwa katika wachezaji ambao alitaka wasajiliwe aliyesajiliwa ni Mrisho Ngassa pekee na wengine uongozi ulishindwa.

Msimu huu simba iliweza kusajili beki Lino Musombo, Kanu Mbiyavanga (Congo), Patrick Ochierg (Kenya) na Komabil Keita (Mali).

Lakini baadaye waliwaacha wachezaji watatu na kumbakiza mmoja Keita kwa madai ya kushindwa kuonyesha uwezo mzuri katika timu yao.

No comments:

Post a Comment