Semina
ya waamuzi na makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) inafanyika Januari 13 na 14 mwaka huu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ndiye anayetarajiwa kufungua semina hiyo.
Wakati
huo huo, Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kimemwalika Rais
Malinzi kuwa mgeni rasmi kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la
Mapinduzi kati ya Simba na Chuoni itakayochezwa kesho (Januari 8 mwaka
huu) saa 2 usiku Uwanja wa Amaan.
No comments:
Post a Comment