M23 |
Waasi wa kundi la 'M23 ' ambalo linapambana kuiangusha serikali ya nchini Congo leo kupitia ukurasa wa wa Twiter wa M23 Congo RDC
waliweza kutoa passport ya askari wa Tanzania ambaye yuko nchini Congo
na askari wengine kwa ajili ya kuisaidia nchi hiyo kupambana na waasi
hao.Tweet hiyo ilionesha kukamatwa kwa askalri huyo akiwa na bunduki
aina ya AK-47 baada ya kutokea mapambano baina ya wanajeshi wanaoisaidia serikali ya Congo na waasi hao. Chini ni ujumbe walioutoa;
“leo Fdlr zikiongozwa na askari toka
Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko
Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri, walizicapa na kuzikimbiza alafu
zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa
cayi na mukate anywe. Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya
kitu, tutamucunga muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC
ambao wanatukanaka hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita,
sisi ni jeshi la Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone
passport ya ule askari ya tanzania ambaye tulikamata”.
No comments:
Post a Comment