http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Sunday, July 21, 2013

WAHITIMU WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI WAASWA KUDUMISHA ULINZI NA MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Gharib Bilal amewataka wahitimu wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi kutumia elimu na maarifa waliyopata kudumisha amani na utulivu nchini.

Akifunga mafunzo ya kwanza ya  Chuo cha Taifa cha Ulinzi jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais Dr. Mohammed Gharib Bilal amesema hafla hiyo imekuja wakati kuna mazingira tata ya kiusalama kimataifa na ndani ya nchi, kama matukio ya hivi karibuni katika Mikoa ya Mtwara na Arusha, ambayo hayakuwahi kutokea katika historia ya Tanzania:

Mapema Mkuu wa Chuo hicho Luteni Jenerali Charles Makakala aliwatunuku tuzo ya Chuo hicho wahitimu hao 20 ambao ni viongozi waandamizi serikalini na asasi za umma:.
Mkuu huyo wa Chuo amesema mafunzo yanayotolewa chuoni hapo yanalenga kuwaandaa viongozi waandamizi wa sekta zote kuwa na mikakati bora ya kulinda na kudumisha usalama wa taifa.

Wakati wa mahafali hayo watu mashuhuri 17 wametunukiwa vyeti maalum vya shukrani kutokana na ushiriki wao katika kufanikisha kozi hiyo. Miongoni mwa waliotunukiwa vyeti hivyo vya shukrani ni pamoja na  Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu  cha Dar es salaam Dr Benson Bana, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara, Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Wananchi -CUF Prof. Ibrahim Lipumba, Prof. na Prof. Reginald Mihanjo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na usalama mhe. Anna Abdallah na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF wamesema Chuo hicho kina umuhimu mkubwa katika ulinzi wa Tanzania.
Miongoni mwa waliohudhuria mahafali hayo ni pamoja na Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mkuu wa Majeshi  Jenerali Davis Mwamunyange, Spika wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Amir Pandu Kificho, mabalozi wa nchi mbalimbali, na viongozi mbalimbali wa serikali.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Gharib Bilal amewataka wahitimu wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi kutumia elimu na maarifa waliyopata kudumisha amani na utulivu nchini.

Akifunga mafunzo ya kwanza ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais Dr. Mohammed Gharib Bilal amesema hafla hiyo imekuja wakati kuna mazingira tata ya kiusalama kimataifa na ndani ya nchi, kama matukio ya hivi karibuni katika Mikoa ya Mtwara na Arusha, ambayo hayakuwahi kutokea katika historia ya Tanzania:

Mapema Mkuu wa Chuo hicho Luteni Jenerali Charles Makakala aliwatunuku tuzo ya Chuo hicho wahitimu hao 20 ambao ni viongozi waandamizi serikalini na asasi za umma:.
Mkuu huyo wa Chuo amesema mafunzo yanayotolewa chuoni hapo yanalenga kuwaandaa viongozi waandamizi wa sekta zote kuwa na mikakati bora ya kulinda na kudumisha usalama wa taifa.

Wakati wa mahafali hayo watu mashuhuri 17 wametunukiwa vyeti maalum vya shukrani kutokana na ushiriki wao katika kufanikisha kozi hiyo. Miongoni mwa waliotunukiwa vyeti hivyo vya shukrani ni pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr Benson Bana, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara, Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Wananchi -CUF Prof. Ibrahim Lipumba, Prof. na Prof. Reginald Mihanjo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na usalama mhe. Anna Abdallah na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF wamesema Chuo hicho kina umuhimu mkubwa katika ulinzi wa Tanzania.
Miongoni mwa waliohudhuria mahafali hayo ni pamoja na Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, Spika wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Amir Pandu Kificho, mabalozi wa nchi mbalimbali, na viongozi mbalimbali wa serikali.

No comments:

Post a Comment