Mastaa wa
soka Ulaya kutembelea magari ya kifahari sio ishu mpya sana na
unaambiwa asilimia kubwa ya club za soka Ulaya huwa wana mikataba na
kampuni za magari kama ilivyo kwa KRC Genk ya Ubelgiji anakocheza Mtanzania Mbwana Samatta ambao wana mkataba na Mercedes Benz.
Unaambiwa KRC Genk wana mkataba na Mercedes Benz ambao kila mchezaji wa klabu hiyo huwa anapewa Benz jipya hata kama atapenda kununua gari kutoka katika kampuni nyingine kama ilivyo kwa Leone Bailey ambaye anatembelea Benz na Range Rover.
Mbwana Samatta bado
hajapewa Benz yake kwa sababu hakufaulu mtihani wa alama za barabarani
kwa kupungukiwa alama nne, kwa sasa anaendeshwa tu na dereva wa klabu
anapokwenda sehemu mbalimbali lakini akifaulu mtihani atapewa kibali cha kuendesha gari Ubelgiji.
No comments:
Post a Comment