Kazi ndogo tu: Pep Guardiola, amesema timu yake haijajiandaa kupiga penati kesho
Alipata
maumivu?: Kocha wa Bayern Munich alipokea maumivu ya kufungwa kwa mara
ya kwanza bao 1-0 katika michezo 53 ya Bundesliga jumamosi dhidi ya Augsburg
................................................................
KOCHA
wa Bayern Munich, Pep Guardiola amesisitiza kuwa klabu yake haijafanya
mazoezi ya kupiga mikwaju ya penati kuelekea mchezo wa marudiano dhidi
ya Manchester United.
Bayern
wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 na
Man Unted dimba la Old Trafford, na kama matokeo kama hayo yatatokea
kesho Allianz Arena, basi mikwaju ya penati itatumika kuamua mshindi.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa kesho,
Gaurdiola amesema timu yake haijafanya maandalizi juu ya mazingira ya
penati.
"Ni masuala ya mbinu tu na kujiamini. Yote yapo kichwani mwa wachezaji wangu". Alisema Gaurdiola.
Guardiola
alisema Man Unted watacheza mpira wa kujihami na kushambulia kwa
kushitukiza, lakini hadhani kama watafikia hatua ya penati.
"Nadhani United watacheza zaidi nyuma. Watataka kucheza zaidi eneo lao na kujilinda".
"Timu za England zinaweza sana kujilinda na kushambulia kwa kushitukiza".
"David Moyes atakuwa na wachezaji 8 mpaka 9 nyuma. Watakuwa wanasubiri tufanye makosa na watushambulie kwa kushitukiza".
"Ndio
maana nasema lazima tuwe na nidhamu kubwa. Tunacheza nyumbani na ni
faida kwetu. Tunalazimika kushambulia vizuri" . Alisema Guardiola.
Guardiola hana wasiwasi na Rooney ambaye anasumbuliwa na majeruhi kama ataweza kuamua matokeo ya Man United usiku wa kesho.
Tabasamu: Wayne Rooney ameonekana mwenye furaha akiwa mazoezini na wachezaji wenzake
Tayari kwa kazi: Rooney akijifua kujiandaa kuwakabili Bayern kesho
Wayne
Rooney amewapa matumaini makubwa Manchester United kuelekea katika
mchezo wa pili wa robo fainali kesho usiku, ligi ya mabingwa barani
Ulaya dhidi ya Bayern Munich baada ya kufanya mazoezi leo hii katika
dimba la Allianz Arena.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, Rooney alishindwa kuitumikia Man United ikishinda
mabao 4-0 dhidi ya Newcastle kwasababu ya majeruhi ya mguu.
Katika
mazoezi ya leo, Ryan Giggs alishiriki baada ya kuwakosa Newcastle,
lakini Marouane Fellaini, aliyetolewa nje katika dimba la St James'
Park kufuatia kuumia, pamoja na Rafael hawakushiriki.
Rooney ameonekana kutougulia maumivu katika mazoezi ya leo kwasababu alionesha juhudi kubwa.
Awali
Kocha wa Man United, David Moyes alisema Rooney alikuwa hatarini
kuukosa mchezo wa kesho baada ya kuumia katika mechi ya sare ya 1-1 Old
Trafford wiki iliyopita, lakini kwasasa inaonekana kutoathirika tena.
Hata hivyo, nyota huyo mwenye miaka 28 atacheza mechi hiyo kubwa zaidi kwa United msimu huu akitumia dawa za kuua maumivu.
Na kocha wa Bayern Pep Guardiola kwa upande wake hakuwa na wasiwasi kuwa Rooney ataikosa mechi ya kesho.
Alisema: 'Rooney anakwenda kucheza kwa asilimia 100. Atacheza, kama mtu anabisha naahidi kumpa zawadi kubwa endapo hatacheza"
Guardiola alimuelezea Rooney kuwa ni mmoja kati ya wachezaji wakubwa aliowaona katika maisha yake ya soka.
Man
United baada ya kuonesha kiwango kizuri katika mchezo wa kwanza,
wanaonekana kuwa na imani ya kufanya kazi vizuri na kusonga mbele dhidi
ya mabingwa hao watetezi.
No comments:
Post a Comment