Huwezi
amini: Akitokea benchi, Demba Ba aliteleza na kupiga mpira uliozama
kimiani na kuiandikia Chelsea bao la pili na la ushindi.
Mwanaume: Demba Ba akishangilia bao lake lililoipeleka Chelsea nusu fainali
Anafunga
safari: Jose Mourinho akikimbia kuelekea eneo la kibendera cha kona
baada ya Chelsea kufunga bao la pili na la muhimu mno usiku huu
Maelekezo: Mourinho akiwaambia wachezaji wake walinde bao hilo la ushindi katika dakika za majeruhi
MSENEGAL
`Supa Sabu` Demba Ba ameibua shangwe, nderemo na vifijo kwa mashabiki
wa Chelsea waliofurika katika dimba la Stamford Bridge usiku huu baada
ya kuifungia klabu yake bao muhimu katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
PSG.
Hii
ilikuwa mechi ya robo fainali ya pili ambayo Chelsea walihitaji ushindi
wa mabao mawili kwa bila ili kufuzu hatua ya nusu fainali kufuatia
kufungwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza nchini Ufaransa.
Chelsea
wamefuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya wastani wa magoli kuwa
3-3, lakini kwa vile wao walifunga bao moja katika kipigo cha 3-1 nchini
Ufaransa wameweza kufuzu hatua ya nusu fainali.
Ba
alifunga bao la pili katika dakika ya 87 na kumfanya Kocha wa Chelsea
Jose Mourinho ashangilie kama alivyofanya miaka ya nyuma akiwa na FC
Porto.
Cesar
Azpilicueta alipiga shuti ambalo liliwababatiza mabeki wa PSG na mpira
kumkuta Ba akiwa eneo zuri na kumalizia kwa ufundi mkubwa mno huku
mlinda mlango,Salvatore Sirigu akibaki hana la kufanya.
Wakati
kila mtu akiamini Mourinho ameshatupwa nje ya mashindano, ghafla baada
ya bao la nyota huyo raia wa Senegal, Jose alikimbia kutoka eneo la
benchi lake kwenda kwenye kibendera cha kona kushangilia na wachezaji
wake.
Mourinho
amewakumbusha watu wengi miaka ya nyuma kwani aliwahi kushangilia kwa
staili hiyo akiwa na FC Porto mwaka 2004 kwenye uwanja wa Old Trafford.
Hakika usiku huu ni wa furaha kubwa kwa Mourinho
kwasababu
kadri muda ulivyozidi kwenda alikuwa anachanganyikiwa na kuona ndoto
zake zinafifia mpaka ilipofika dakika hizo za lala salama na Ba
kumnyanyua kwa shangwe.
Bao la kwanza la Chelsea lilifungwa na Mjerumani Andre Schurrle katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza.
Katika
mechi nyingine, Real Madrid wamefuzu hatua ya nusu fainali licha ya
kufungwa mabao 2-0 na Borrusia Dortmund katika dimba la Signal Iduna
Park.
Madrid wamenusurika kutokana na ushindi wa mabao 3-o walioupata Santiago Bernabeu katika mchezo wa kwanza.
Real wakianza bila ya Cristiano Ronaldo ambaye hakuwa fiti kuanza mchezo wa leo, walikaribia kutolewa na
vijana wa Jurgen Klopp, lakini jitihada za mlinda mlango wao, Iker Casillas zimewaepushia balaa la kutolewa.
Hata
hivyo, Real Madrid walikosa penati baada ya winga wake nyota, Angel Di
Maria kuteleza wakati akipiga tuta hilo, hivyo kipa wa Borussia kuokoa
kirahisi.
Hayajatosha: Marco Reus ameifungia mabao mawili Borussia Dortmund, lakini wametolewa na Real Madrid
Bahati
kubwa: Kipa wa Borussia, Roman Weidenfeller akiokoa penati ya Angel Di
Maria baada ya nyota huyo raia wa Argentina kuteleza wakati anapiga
mpira
Haamini: Cristiano Ronaldo akiduwaa baada ya Di Maria kukosa tuta
Wamekosa bahati: Dortmund walipata nafasi nyingi za kufunga zikiwemo tatu za Henrikh Mkhitaryan
No comments:
Post a Comment